Nyumbani » Mandela Akumbukwa Wewe ni browsing entries tagged na “Mandela Akumbukwa”

Baraza Kuu lamkumbuka Nelson Mandela

Kusikiliza / Hayati Nelson Mandela akiwa Umoja wa Mataifa wakati akiwa Rais(1994)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao maalumu cha kumkumbuka Hayati Nelson Mandela, siku chache baada ya kuzikwa kwake siku ya Jumapili. Joshua Mmali na taarifa kamili (TAARIFA YA JOSHUA) "Tumekusanyika hapa leo kumuenzi mtu ambaye si wa kawaida, Nelson Mandela. Mtu ambaye alitoa msukumo kwa taifa lake, bara na ulimwengu mzima kupitia [...]

19/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP imetoa wito wa kumuenzi Nelson Mandela kwa kutokomeza njaa:

Kusikiliza / Soko la mboga dar Es Salaam

  Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) Ertharin Cousin Alhamisi ametoa wito wa kumuenzi hayati Nelson Mandela kwa kutokomeza njaa katika watu wetu. Bi Cousin  ameyasema hayo mjini Dar Es Salaam, Tanzania wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuwawezesha wakulima wadogowadogo kupata fursa ya huduma za fedha kama akaunti za benki, kadi [...]

12/12/2013 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakati Mandela akipumzika kwa amani ni wakati wa kumuenzi kwa vitendo:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu, UM Ban Ki-moon na picha ya hayati Nelson MAndela(picha ya UN/MArio Salerno

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameungana na mamilioni ya watu wa Afrika ya Kusini, familia ya Marehemu Nelson Mandela, viongozi mbalimbali , watu mashuhuri na dunia kwa ujumla kutoa heshimazake za mwisho kwa jabali la Afrika na mtetezi wa haki duniani mzee Madiba, Nelson Mandela. Assumpta Massoi na taarifa kamili (MUSIC) Hivyo [...]

10/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Ban amsifu Mandela kama jabali wa haki na usawa

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwa Afrika Kusini katika Ukumbusho wa Nelson Mandela

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, ambaye yuko Afrika Kusini, amemsifu tena Hayati Mzee Nelson Mandela kama mtu aliyekuwa jabali wa haki, usawa na haki za binadamu. Akizungumza kwenye kituo cha ukumbusho cha Nelson Mandela, Bwana Ban amesema kuwa Nelson Mandela alikuwa zaidi ya mmoja wa viongozi wenye hadhi ya juu zaidi [...]

09/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Kuhudhuria ibada ya kuomboleza kifo cha Mandela Jumanne

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ataondoka mjini Paris Ufaransa kuelekea Afrika Kusini hapo kesho Jumapili, ili kuhudhuria ibada rasmi ya maombolezo ya Hayati Mzee Nelson Mandela, ambayo itafanyika mnamo siku ya Jumanne. Bwana Ban ambaye amekuwa Ufaransa kuhudhuria mkutano kuhusu amani Afrika, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa kuna haja [...]

07/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kosa lililomfanya Mandela afungwe ni kupigania Haki:Mbotela

Kusikiliza / Mambo Mbotela na Nelson Mandela

Mzee Mandela ni kiongozi ambaye anatambulika kote ulimwenguni, umaarufu wake atakumbukwa na wengi hususani wale waliomshuhudia. Miongoni mwao ni mwandishi mashuhuri Afrika Mashriki Leornard Mambo mbotela kutoka Kenya. Jason Nyakundi amefanya mahojiano maalum na Mambo mbotela kuhusu wasifu wa hayati Nelson Mandela. Kwanza Mambo annanza kueleza vile ufahamu wake wa Mandela (MAHOJIANO YA JASON NA [...]

07/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mandela Akumbukwa na watu mbali mbali duniani

Kusikiliza / nm3

  Mnamo Alhamisi Disemba 5 Nelson Mandela alifariki huko Afrika kusini akiwa na umri wa miaka 95. Kifo chake kimehuzunisha ulimwengu mzima kwani alikuwa  kiongozi  mashuhuri na mtetezi wa haki za bindamu ambaye alifahamika na kusifika kote ulimwenguni. Basi katika kumbuka Mzee Mandela, ungana na Joshua Mmali kwa makala ifuatayo Oktoba 1994. Rais wa kwanza [...]

06/12/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mzee Nelson Mandela hakuwa mtu wa kujikuza: Naibu Mkuu UNAMA

Kusikiliza / Nicholas Haysom, Naibu Mkuu wa UNAMA ambaye aliwahi kuwa Mshauri Mkuu wa masuala ya sheria wa Mzee Mandela

Nicholas Haysom, raia wa Afrika Kusini ambaye alifanya kazi ya Mshauri Mkuu wa masuala ya Sheria kwa Mzee Nelson Mandela wakati wa kipindi chake chote cha Urais na hata baada ya kustaafu wadhifa huo, amesema Madiba hakuwa mtu wa kujikuza. Haysom ambaye kwa sasa ni Naibu Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchiniAfghanistan, [...]

06/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Rais Mstaafu wa Tanzania aungana na dunia kumuenzi Mzee Mandela

Kusikiliza / Mzee Mandela akitambulishwa na Mwl Nyerere kwenye uwanja wa Taifa jijini DSM wakati wa ziara nchini Tanzania

Madiba amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 na ulimwengu mzima umegubikwa na machozi! Kumbukumbu ya kile alichofanyia ulimwengu huu kuhakikisha maisha yanakuwa bora kwa wengi hususan huko Afrika Kusini na hata kugusa maisha ya wananchi wengine, hakitosahaulikaAbadan! Joshua Mmali katika ripoti hii fupi anaangazia kumbukumbu ya  Mzee Madiba!

06/12/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kifo cha Mandela: Burundi yatangaza siku tatu za maombolezo

Kusikiliza / Mzee Mandela akilakiwa na aliyekuwa Rais wa Burundi Pierre Buyoya mjini Bujumbura mwaka 2003

Burundi imetangaza  siku tatu za maombolezo kufuatia kifo cha mzee Nelson Mandela. Mandela atakumbukwa katika nchi hiyo kutokana na jukumu  lake la kuwasuluhisha warundi baada ya mgogoro wa muda mrefu na kufikia makubaliano ya Arusha ambayo ni  msingi wa  taasisi za nchi hiyo na utengamano wa taifa. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA ametuandalia [...]

06/12/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kifo cha Mzee Mandela, bendera ya UM yapepea nusu mlingoti

Kusikiliza / Bendera ya UN yapeperushwa nusu mlingoti kwa ajili ya Mandela

Majonzi, huzuni vimeendelea kughubika ulimwengu kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela, aliyefahamika kutokana na ujasiri wake wa kupigania haki kwa maslahi ya wanaokandamizwa. Ndani ya Umoja wa Mataifa ambako misingi inayosimamiwa ya haki, amani, ulinzi na usalama Mzee Mandela aliipigania, saa Nne Asubuhi bendera za mataifa ya nchi wanachama kwenye makao makuu mjiniNew Yorkzilishushwa huku [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yasema Mandela hakutaka ukiukwaji wa haki

Kusikiliza / ICC

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko The Hague, imeungana na watu wa Afrika ya Kusini, bara la Afrika na jumuiya ya kimataifa kuombeleza kifo cha jabali wa Afrika, Mzee Nelson Mandela aliyekuwa sauti ya usawa na haki. ICC imesema ni wakati utawala wa Mandela mnamo Julai 17 mwaka 1998 nchi ya Afrika ya Kusini [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mandela alifuata maadili kuliko kiongozi yeyote wa zama za sasa: Pillay

Kusikiliza / Hayati Nelson Mandela

Mzee Madiba , Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela aliyeaga dunia Alhamisi anatambulika kama kinara wa uhuru, usawa na haki za binadamu. Hayo yamesemwa na Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navi Pillay aliyeongeza kuwa Mandela pengine ndiye kiongozi mfuata maadili kuliko mwingine yeyote katika kizazi hiki. Amesema [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya wasema Mzee Mandela hakuna wa kulinganishwa naye

Kusikiliza / Mzee Mandela alipotembelea Kenya mara tu baada ya kutoka gerezani

Nchini Kenya Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wake wametoa salamu kwa Taifa la Afrika Kusini, familia na wananchi kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela, na hiyo ni katika salamu za rambirambi na maoni yao kama anavyoripoti mwandishi wetu wa Nairobi, Jason Nyakundi. (Ripoti ya Jason) Kifo cha Mzee Mandela kimegusa wengi siyo tu Afrika Kusini [...]

06/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mandela alitetea maadili ya haki na maridhiano: Rais Baraza la usalama

Kusikiliza / Baraza la Usalama wakati wa dakika moja ya kumkumbuka Mandela

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo walilazimika kusitisha kikao chao cha kupokea ripoti kuhusu mahakama za za uhalifu wa kimbariRwanda, ICTR na mahakama ya uhalifu ya taifa la zamani laYugoslavia, ICTY ili kuugana na ulimwengu kwenye maombolezo ya kifo cha Mzee Nelson Mandela. Wajumbe walisimama kwa dakika moja kumkumbuka Mzee na [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nelson Mandela afariki dunia: Ban atuma rambirambi

Kusikiliza / Nelson Mandela

Nelson Mandela, Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 95.  Kifo cha Mandela kimetangazwa na Rais Jacob Zuma kupitia televisheni ya nchi hiyo. Kufuatia kifo hicho Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza na waandishi wa habari mjini New York..  (Sauti ya Ban Ki-Moon) "Nimesikitishwa sana na [...]

05/12/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Wananchi wa Burundi wamuenzi Mandela kwa msaada wake

Kusikiliza / mandela

Mnamo tarehe 18 Julai wiki hii, ulimwengu mzima uliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mandela, ili kumuenzi Nelson Mandela, rais wa zamani wa Afrika Kusini na Shujaa wa kupigania uhuru na haki za binadamu. Hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ilifanyika hafla maalum ya kuadhimisha siku hiyo kwenye ukumbi wa mikutano ya Baraza Kuu, [...]

19/07/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mandela amwagiwa sifa na viongozi Afrika

Kusikiliza / Nelson Mandela

Katika kuadhimisha Siku hii ya Kimataifa ya Mandela, viongozi mbali mbali wa zamani kutoka Afrika wamekuwa wakielezea sifa za Mandela wakikumbuka mchango wake katika maisha ya mwanadamu. Miongoni mwao ni Rais mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi(CLIP MWINYI) Mwingine aliyemtolea Nelson Mandela sifa kem kem ni Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu [...]

18/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Kimataifa ya Mandela

Kusikiliza / Nelson Mandela akizungumza - Baraza Kuu la UM

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, shujaa wa kupigania uhuru Afrika Kusini na mpiganiaji haki za binadamu, ambaye leo ikiwa siku ya kuzaliwa kwake, amehitimisha miaka 95. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeadhimisha siku hii kwa kuangalia video fupi ya Mandela, akiongea nyakati tofauti, ukiwemo mwaka 1990, alipotoa hotuba kwenye Umoja wa [...]

18/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafanyakazi wa UM wamuenzi Mandela kwa kuwasaidia waathirika wa Sandy

Kusikiliza / Wafanyi kazi wa UM

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Mandela Umoja wa Mataifa unaungana na wito wa wakfu wa Mandela wa kutaka watu "kuchukua hatua na kuchagiza mabadiliko" wito ambao unawataka watu kujitolea kwa dakika 67 ili kuwasaidia wengine katika sehemu mbalimbali ikiwemo hospital, kufundisha watoto, kugawa chakula kwa wasio na makazi ,au shughuli yoyote ya huduma kwa [...]

18/07/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya Mandela ni wakati wa kuchukua hatua na kuyakumbuka aliyotenda:Ban

Kusikiliza / Siku ya Mandela Julai 18

Watu duniani kote wanachagizwa kuchukua hatua kwa niaba ya wengine Alhamisi ya leo katika kusherehekea siku ya kimataifa ya Nelson Mandela. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa Ban Ki-moon ambaye anaadhimisha siku hii kwa kukumbuka maisha na mchango mkubwa wa kiongozi huyo wa kimataifa ambaye kwa sasa bado yuko mahututi hospitali. [...]

18/07/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Akizungumzia kuchanuka kwa Afrika Ban pia akumbuka afya ya Mandela

Kusikiliza / Nelson Mandela, (picha ya maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mmoja wa majabali ya Afrika kwa karne ya 20 Mzee Nelson Mandela yu mahututi hospitali na kusema kuwa mawazo na sala za kila mmoja zinaelekezwa kwake, familia yake, watu wa Afrika ya Kusini na dunia nzima ambao wameguswa na ujasiri na maisha yake. Flora Nducha anaripoti(RIPOTI [...]

27/06/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031