Ripoti yenye mada inayosema: Njaa, Maafa na Matumaini: Tafakari mpya juu ya huduma za misaada ya kiutu katika Afrika ilihimiza mashirika yatoayo misaada ya kihali, pamoja na serikali za nchi husika zifanye mapitio juu ya namna misaada inavyofadhiliwa na kuwasilishwa kwenye maeneo hayo, na pia kushtumu kwamba mfumo wa sasa wa kugawa misaada huwa unategemea huduma za kudhibiti maafa baada ya kutukia, badala ya kuandaa mipango kinga dhidi ya athari za maafa, hali ambayo inaaminika huyanyima mataifa ya Afrika suluhu za kudumu kukabili dharura za kimaumbile; mazingira ambayo vile vile huyafanya mashirika yanayohudumia misaada ya kiutu kushughulikia zaidi taratibu za kuomba kufadhiliwa mara kwa mara misaada ya kuhudumia waathirika wa maafa.