Kadhalika, mtayraishaji vipindi wa Idhaa ya Kiingereza ya Redio ya UM, Derrick Mbatha, naye pia alipata fursa ya kumhoji Dktr Mayaki kuhusu masuala yanayoambatana na miradi ya kukuza maendeleo ya kiuchumi na jamii katika Afrika, kwa ushirikiano na wadau wa kimataifa, ikijumlisha mashirika ya UM. Tulitaka kujua kama nchi za KiAfrika zinaelekea mkondo unaoridhisha katika kutekeleza miradi ya maendeleo, kwa hivi sasa, hasa katika kipindi ambacho uchumi wa dunia umezongwa na matatizo aina kwa aina, ikijumlisha mizozo ya kifedha, chakula na athari haribifu zamabadiliko ya hali ya hewa. Kwenye mahojiano na Mbatha, miongoni mwa mada alizogusia ilijumlisha namna mataifa ya Afrika yanavyotekeleza miradi ya maendeleo; matatizo ya uhamaji wa kutoka mashamba kwenda mijini na umuhimu wa kuimarisha miundombinu, kwa minajili ya kukuza maendeleo ya vijijini.
Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaaya mtandao.