Azimio la Wazo la kuwasilisha 'Wajibu wa Kulinda Raia' lilipitishwa mwezi Septemba 2005 kwenye Mkutano wa Kimataifa, ambapo viongozi 170 ziada, walikubaliana ya kuwa wanawajibika kuimarisha maisha bora, kwa siku za baadaye, kwa kila mwanadamu, kote ulimwenguni. Waliafikiana kwamba ni kweli ni dhamana ya kila Taifa kuhami na kuwalinda raia dhidi ya mauaji ya halaiki, na kuwakinga na madhara ya makosa ya vita pamoja na kuwahami na jinai dhidi ya utu, na dhidi ya hatari ya vita vya utakaso wa mila za kijadi (ethnic cleansing). Lakini wajumbe wa kimataifa vile vile walikubaliana pindi wenye mamlaka ya Kitaifa watashindwa, au hukosa uwezo wa kuwakinga raia dhidi ya jinai hizo, au wakishindwa kukomesha makosa hayo ya kiutu dhidi ya raia, jumuiya ya kimataifa itawajibika na kulazimika kuchukua hatua za dharura, kipamoja, kwa ridhaa ya wenye madaraka, kuhami raia hawo dhaifu, dhidi ya hatari ya kuangamizwa, kwa kutumia kanuni iliozingatiwa kwenye Baraza Kuu, iliotambuliwa kama "wajibu wa kulinda raia" au kwa umaarufu wake huitwa 'kanuni ya R2P'.
Sikiliza mahojiano kamili baina ya mwendesha vipindi wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM na Profesa Ngugi wa Thiong'o kuhusu 'kanuni ya R2P'.