Ahadi hii ilitolewa manmo siku ya mwisho ya kikao cha viongozi wa Kundi la G-8 na ilikaribishwa na mashirika kadha ya UM. Jacques Diouf, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO), ambaye vile vile alihudhuria Mkutano wa G-8, alinakiliwa akisema "msaada wa chakula ni kadhia muhimu sana kwa zile nchi masikini ambazo, kwa sasa, vile vile zimezongwa na matatizo ya ukame, mafuriko, fujo na vurugu, na husumbuliwa sana na tatizo la chakula cha kunusuru maisha."