Matangazo ya Radio ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya simu

Matangazo ya Radio ya Umoja wa Mataifa kwa lugha Nane sasa yanapatikana saa 24 kila siku. Matangazo kuhusu shughuli za Umoja huo kuanzia taarifa za habari, makala, mahojiano, mikutano na waandishi wa habari na mikutano ya moja kwa moja waweza kuyapata kwa lugha uitakayo kati ya hizo nane kwa kupiga nambari ya simu kupitia simu yako ya kiganjani au ya mezani. Huhitaji programu maalum au hata kifurushi cha data! Unachohitaji ni muda wa maongezi! Hivyo basi  ukiwa Marekani piga namba zifuatazo:

Idhaa ya Kiarabu          : 712-432-9912

Idhaa ya Kichina          :712-432-9911

Idhaa ya kiingereza:  : 712-432-9910

Idhaa ya Kifaransa      :712-432-9913

Idhaa ya Kiswahili      :712-432-9916

Idhaa ya Kireno            :712-432-9917

Idhaa ya Kirusi             :712-432-9914

Idhaa ya Kihispania     :712-432-9915

Matangazo ya Radio ya Umoja wa Mataifa kupitia AudioNow yatasambaa zaidi maeneo mengine punde!  Sikiliza Radio ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya simu Wakati Wowote!

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031