Idhaa ya Redio ya UM

Novemba 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kuunganisha

Huduma

 20 Novemba 2009
Real Chapisha

Ripoti ya Hali ya Watoto Duniani 2009 - UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limewasilisha ripoti muhimu Alkhamisi inayosailia: Hali ya Watoto Duniani.

Ripoti ya mwaka huu imemurika juu ya athari za utekelezaji wa Mkataba wa Haki za Mtoto - kanuni ambazo 2009 zitakamilisha miaka 20 tangu Baraza Kuu la UM kupitisha Mkataba. Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Ann Veneman alisema Mkataba wa Haki za Mtoto umerekibisha hisia ya utambuzi mzuri zaidi wa mahitaji ya watoto na haki zao katika ulimwengu. Kwa mujibu wa ripoti, kuanzia miaka 20 iliopita hadi hivi sasa maendeleo makubwa kadha yalipatikana kwenye uetekelezaji wa haki za watoto; kwa mfano, udhibiti wa vifo vya watoto ulionekana kufanyika kwa kiwango cha kutia moyo katika maeneo mbalimbali ya dunia; vile vile idadi kubwa ya watoto waliandikishwa kuhudhuria skuli za pramiari katika kipindi cha miaka 20, na vitendo vya kuajiri watoto wadogo kushiriki kwenye mapigano vilishuhudiwa kupungua, wakati utoroshaji wa watoto kutoka makwao na kuvushwa mipaka kushiriki kwenye vibarua vya kulazimishwa, vitendo hivi navyo vimepungua katika miaka ya karibuni.