20 Novemba 2009
TBD
IOM imetangaza kuwapatia IDPs wa Zimbabwe hifadhi na misaada ya dharura
20/11/2009
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuanzisha mradi mpya wa kuwasaidia kidharura wahamiaji wa ndani (IDPs) waliong'olewa makazi katika Zimbabwe kupata hifadhi wanayohitajia kumudu maisha.
Mradi huu unatarajiwa kuwahudumia raia 18,000 waliong'olewa makazi - sawa na aila 3,000 - kutoka yale majimbo mawili muhimu ya Zimbabwe ya Harare na Mashonaland ya Kati ambayo yalihujumiwa na mawimbi makali ya kufurushwa makazi watu katika 2008 kutokana na vurugu la kisiasa liliopamba nchini wakati huo, pamoja na zile sera za kunyakua mashamba ya wapinzani, ambazo zilisababisha watu kadha kunyimwa mahali pa kukaa.

