Idhaa ya Redio ya UM

Novemba 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kuunganisha

Huduma

 20 Novemba 2009
Real Chapisha

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon ameripotiwa kukaribisha uteuzi wa Herman van Rompuy kuwa raisi wa awali wa Umoja wa Ulaya, na vile vile kupongeza uteuzi wa Catherine Ashton kuwa Mjumbe Mkuu wa Umoja wa Ulaya juu ya Masuala ya Nchi za Kigeni na Sera za Usalama. KM alisema atashirikiana kikazi, kwa ukaribu, na viongozi hawa wa Umoja wa Ulaya, yaani Rompuy na Ashton, na kuimarisha uhusiano baina ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.

Ijumaa asubuhi, KM alifungua rasmi sherehe maalumu kwenye Makao Makuu ya UM, kuadhimisha miaka 20 tangu Mkataba wa Haki za Mtoto ulipoidhinishwa na Mataifa Wanachama. Kwenye hotuba ya ufunguzi, KM alisema Mkataba wa Haki za Mtoto ulitambua, kwa mara ya kwanza kwamba, kimsingi, watoto wote wamebarikiwa haki halali kote ulimwenguni, na wanahitajia ulinzi unaofaa kimaisha. Aliongeza kusema, katika kipindi cha miaka 20 iliopita, Mkataba wa Haki za Mtoto ulisaidia kuongoza nchi wanachama kulea na kuwapatia hifadhi wanayostahiki fungu la jamii, lilio dhaifu zaidi kihali, na ambalo hujumlisha umma wenye umri mdogo. Alisema Mkataba wa Haki za Mtoto ulikuwa ni chombo cha sheria ya kimataifa juu ya haki za binadamu, kilichofanikiwa kuidhinishwa na idadi kubwa ya nchi wanachama - mataifa 193 - na ulisaidia kuhamasisha mwelekeo mpya na maendeleo katika kuilimisha watoto na kuwanusuru kimaisha.

Alkhamisi, KM alihutubia kikao kisio rasmi cha Baraza Kuu ambacho kilijadilia mabadiliko ya hali ya hewa. Kwenye kikao hiki, KM alisema licha ya kuwa kuna tetesi zinazojigamba Mkutano wa Copenhagen juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa utamalizikia na "masikitiko makali" bila ya itifaki ya kuridhisha, hata hivyo, anaamini kihakika kwamba wajumbe wa kimataifa watakaokusanyika Copenhagen watafikia mapatano yatakayosaidia kuandaa "mkataba mpya wenye masharti ya kisheria katika 2010" utakaosaidia umma wa kimataifa kudhibiti bora taathira za mabadiliko ya hali ya hewa. Alisema kila siku alishuhudia mwelekeo wenye kasi ya kisiasa unatekelezwa na mataifa, wenye kubashiria itifaki juu ya udhibiti wa hali ya hewa itakamilishwa, kwa wakati - alitoa mfano wa ahadi za Marekani na Uchina kwamba wapo tayari kushirikiana kipamoja kwenye kikao cha Copenhagen; wakati Indonesia imetangaza itapunguza umwagaji wa hewa chafu kwa asilimia 26; na Urusi pia kueleza kuwa ipo tayari kupunguza hewa chafu kwa asilimia 25 katika 2020, pindi mataifa mengine yatakubali vile vile kuyatekeleza hayo. Ishara hizi, alitiliza mkazo KM, ni hatua za kutia moyo kwamba jumuiya ya kimataifa ina fursa ya kufikia mapatano ya kuridhisha itakapojumuika Copenhagen kusailia udhibiti wa pamoja waw mabadiliko ya hali ya hewa.