Idhaa ya Redio ya UM

Novemba 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kuunganisha

Huduma

 19 Novemba 2009
Real Chapisha

Mashirika ya UM yanahudumia kihali WaAngola waliofukuzwa kutoka JKK

Ofisi ya OCHA imeripoti raia wa Angola waliofukuzwa JKK na waliorejea nchini mwao hivi sasa wanajumlisha watu 51,000.

Kwa mujibu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), na taarifa za Serikali ya JKK, thuluthi mbili ya raia hawo walikuwa ni wahamaji. OCHA imeripoti pia wahamaji 30,000 ziada walifanikiwa kurejeshwa kwenye mastakimu yao ya asili. Kadhalika iliripotiwa ya kuwa timu ya watumishi wa UNHCR waliopelekwa Jimbo la Zaire kutathminia mahitaji ya kimsingi kwa wahamiaji waliorejeshwa makwao, hawakuruhusiwa kuzifikia zile sehemu za makazi ya wahamiaji husika kuanzia tarehe 05 Septemba hadi sasa hivi, hatua ambayo haitowawezesha kusajili wahamiaji hawo kama inavyotakikana kisheria. Mashirika mengine ya UM, yale yanayohusikana na watoto, UNICEF na huduma za maendeleo ya chakula na kilimo, FAO yanashirikiana kupeleka misaada ya mahema, mablangeti, mikeka ya kulalia na biskuti zenye nguvu ya kurtubisha afya kuhudumia wahamiaji, na vile vile kuwapatia wale wahamiaji wakulima mbegu na vifaa vya kulimia ili kuhakikisha watajitegemea chakula kwa siku za baadaye.