Idhaa ya Redio ya UM

Novemba 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kuunganisha

Huduma

 19 Novemba 2009
Real Chapisha

MONUC imekaribisha kukamatwa Ujerumani kwa viongozi wawili wa FDLR

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limetangaza kukaribisha kukamatwa nchini Ujerumani, mnamo siku ya Ijumanne, kwa viongozi wawili wa kundi la waasi la FDLR (Forces démocratiques de Libération du Rwanda), wanaoitwa Ignace Murwanashyka and Straton Musoni.

MONUC

MONUC

MONUC ilieleza kukamatwa kwa viongozi hawa kutasaidia kwenye zile juhudi za pande nyingi - zenye mwelekeo wa kidiplomasiya, kisiasa na kijeshi - na kuwaaminisha wafuasi wa FDLR kamba wakati umeshawadia kwa wao kusalimisha silaha zao, na kuhama nchi kwa sababu kuwepo kwao katika JKK ni kitendo kisio halali.