Idhaa ya Redio ya UM

Novemba 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kuunganisha

Huduma

 19 Novemba 2009
Real Chapisha

Uspeni imeongeza maradufu mchango wake kwa WFP kupambana na njaa katika Pembe ya Afrika

Soraya Rodriguez Ramos, Waziri wa Nchi wa Uspeni kwa Ushirikiano wa Kimataifa, ametangaza siku ya leo kuwa serikali yao imekabidhi Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) msaada wa Yuro milioni 75 (dola milioni 112) kutumiwa kufarajia hali mbaya ya chakula iliolivaa eneo la Pembe ya Afrika.

Tangazo hili lilitolewa kufuatia Mkutano Mkuu juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula Duniani, uliomalizika juzi kwenye mji mkuu wa Utaliana. Mchango wa Uspeni kwa WFP kwa sasa umezidi mardufu. Waziri wa Nchi wa Uspeni alitilia mkazo kwenye taarifa yake kwamba Mradi Mkuu wa Maendeleo wa taifa lake hutilia mkazo zaidi kwenye umuhimu wa kutoa misaada kila inapohitajika, bila kujali ni mazingira ya aina gani nchi mfadhili hukabiliwa nayo. Alisisitiza kwamba "wakati mizozo inapotukia, ndipo misaada ya maendeleo inapohitajika zaidi kushinda wakati wowote mwengine, kwa sababu katika kipindi hicho umma muhitaji ndio huumia zaidi na sababu za kiuchumi na hutegemea kufadhiliwa misaada ya kihali kidharura kutoka wahisani wa kimataifa."