TBD
Sheria kali lazima zitekelezwe kuhifadhi mali ya asili kwenye mazingira ya mapigano, inasema ripoti ya UNEP
Shirika la UM juu ya Hifadhi ya mazingira (UNEP) limechapisha ripoti mpya, ilioandaliwa na wataalamu wa sheria, inayozingatia kanuni zinazohitajika kubuniwa na kuimarishwa ili kutunza mazingira, wakati wa mapigano, uhasama, vurugu na vita.
Ripoti ilitilia mkazo kwamba sheria ziliopo sasa hivi za kuhifadhi mazingira haziridhishi, na zinahitajia kuimarishwa kwa makusudio ya kutunza vizuri zaidi mali ya ya asili ya kwenye eneo lenye mapigano, kama inavyostahiki. Ripoti ilihadharisha, licha ya kuwa Itifaki Ziada ya Awali ndani ya Mkataba wa Geneva, inazingatia suala la kuhifadhi mazingira, kauli iliomo kwenye sheria hiyo ni "kali sana na sio sahihi". Wataalamu wa sheria wamependekeza kwenye ripoti ya UNEP kuwepo usahihi unaofahamika kwenye kanuni za kuhifadhi mali ya asili unaoelezea, kidhahiri, kiwango cha eneo za mamia ya kilomita za mraba, ambazo hutafisiriwa ni mali ya asili, na uharibifu utakaozuka hapo kwa kipindi cha miezi kadha au katika majira fulani, utamaanisha unyonyaji haramu na uharibifu wa rasilmali. Mapendekezo mengine ya ripoti inajumlisha mapendekezo ya kuunda chombo kipya cha sheria kitakachokataza shughuli za kijeshi kufanyika kwenye eneo la hifadhi ya mazingira, na kutunza mfumo wa ikolojia unaotegemewa kiuchumi na kijamii, kama utunzaji wa mahandaki ya maji chini ya ardhi, maeneo ya kilimo na machungani, bustani za mbuga, misitu ya taifa na makazi ya wanyama wanaohatarishwa kuangamia.

