5 Novemba 2009
TBD
Kesi ya Bemba itaanzishwa rasmi Aprili 2010 mjini Hague: ICC
05/11/2009
Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) imetangaza kwesi ya Jean-Pierre Bemba itaanza kusikilizwa rasmi mwezi Aprili mwaka 2010.
Bemba ametuhumiwa makosa mawili dhidi ya utu na makosa matatu ya vita, jinai ilioendelezwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, baina ya miezi ya Oktoba 2002 na Mchi 2003, na kundi aliloliongoza la Chama cha Ukombozi wa Kongo (Mouvement de libération du Congo). Bemba alishikwa mwezi Julai na polisi wa Ubelgiji na baadaye alihamishwa kwenye Mahakama ya ICC iliopo kwenye mji wa Hague, Uholanzi, akisubiri kesi.

