Idhaa ya Redio ya UM

Novemba 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kuunganisha

Huduma

 5 Novemba 2009
Real Chapisha

Wafanyakazi wa UNAMA Afghanistan watahamishiwa makazi ya muda kupata usalama

Shirika la UM la Kuisaidia Afghanistan (UNAMA) limetangaza kuwa litawahamisha baadhi ya wafanyakazi wake na kuwapeleka kwenye makazi ya muda, ndani ya nchi au nje ya Afghanistan,

ikiwa miongoni mwa hatua ziada za usalama zinazochukuliwa na UM, kufuatia mashambulio maututi yaliojiri wiki iliopita mjini Kabul, ambapo watumishi watano wa UM waliuawa na wenziwao kadha wengine walijeruhiwa. Taarifa iliotolewa kwa waandishi habari, imeeleza kwamba "kuanzia hivi sasa, UM unachukua hatua ziada za kupunguza hatari kwa usalama wa wafanyakazi wa kizalendo na wale wa kimataifa waliopo Afghanistan." Uamuzi huu umechukuliwa kufuatia shambulio la tarehe 28 Oktoba dhidi ya watumishi wa UM katika Kabul, pamoja na matishio ya kuua yaliokusudiwa wafanyakazi wa UM, ambayo yanaendelea kupigiwa mbiu na makundi adui mbalimbali. Kwa kulingana na taarifa za Shirika la UNAMA, kundi la Taliban ndio liliodai kuhusika na shambulio la wiki ya jana kwenye nyumba za wageni mjini Kabul, walipokuwa wakiishi wafanyakazi 34 wa UM. Watu karibu 6,000 hivi sasa wanaitumikia UM katika maeneo mbalimbali ya Afghanistan, ikijumlisha wafanyakazi wa UM 1,100 waliotoka nchi za nje.