TBD
Mvua kali Kenya zimewanyima makazi maelfu ya raia
Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imechapisha taarifa iliobainisha baadhi ya maeneo katika Kenya, hivi sasa yamepigwa na mvua kubwa kabisa, yenye taathira mbaya kieneo, licha ya kuwa sehemu kubwa ya nchi babdo inaendelea kusumbuliwa na athari za ukame uliotanda kwa muda mrefu huko katika kipindi cha karibuni.
Watu wanaokadiriwa 4,600 wanaoishi maeneo ya mwambao wa Bahari ya Hindi na katika sehemu za majimbo ya kaskazini-mashariki wameng'olewa mastakimu, na hulazimika kutafuta hifadhi ya muda katika maskuli na nyumba za wenyeji waliopo nje ya maeneo yao. Watawala wenyeji, wa maeneo yanayopokea wahamiaji walioghumiwa na mvua kali, wakisaidiwa na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) wamefanikiwa, kwa sasa, kutia dawa ya kuua vijidudu kwenye sehemu moja ya nchi ambapo visima kadha viliambukizwa na maji machafu ya mafuriko. UM una wasiwasi watu 750,000 Kenya huenda wakaathirika, kihali, na mafuriko mabaya pamoja na maporomoko ya ardhi yanayopaliliwa na hali ya hewa ya El Nino ilioshatadi katika miezi ya Oktoba, Novemba na Disemba.

