TBD
Viongozi wa kidini na wasio wa kidini wanasihiwa na KM kuhusu ulazima wa kudhibiti kipamoja taathira za mabadiliko ya hali ya hewa
Kadhalika, Ijumanne, KM Ban Ki-moon alihutubia mkusanyiko wa viongozi wa kidini na wale wasiohusiana na dini, katika Kasri ya Windsor, juu ya ulazima wa kushughulikia kipamoja matatizo yanayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.
Alisema jamii za kimataifa za kidini zinatunza nafasi muhimu katika majadiliano yanayohusu majaaliwa ya sayari ya ulimwengu wetu kwa siku za baadaye, na hatari ya maisha inayoletwa na kasi ya uharibifu wa mabadiliko ya hali ya hewa. Aliwaambia viongozi hawo kwamba ni wajibu wetu sote kupunguza taathira za hewa chafu inayomwagwa angani, na ni lazima kuusaidia umma dhaifu na maskini ulimwenguni kujirekibisha kimaisha, ili kujikinga na madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa. KM alisema hivi sasa tumefikia kipindi muhimu katika historia ya walimwengu juu ya udhibiti wa athari haribifu za mabadiliko ya hali ya hewa. Vile vile alihadharisha kwenye taarifa aliotoa kabla ya hapo, Ijumatatu usiku, kwamba wale wanaolalamika juhudi za kukabili mabadiliko ya hewa ni huduma zenye gharama nyingi wakumbuke pia kama hatujadhibiti hivi sasa, uharibifu unaoletwa na hali ya hewa, tutatalipa thamani kubwa mno katika miaka ya baadaye.

