Idhaa ya Redio ya UM

Novemba 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30

Kuunganisha

Huduma

 2 Novemba 2009
Real Chapisha

Wahalifu wanane wa makosa ya vita Sierra Leone wahamishiwa kifungoni Rwanda

Wahalifu wanane waliopatikana na hatia ya kushiriki kwenye jinai ya vita na makosa dhidi ya utu, na Mahakama Maalumu juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone (SCSL), Ijumaa walisafirishwa kutoka vituo vya kufungia watu viliopo Freetown, Sierra Leone na kuhamishiwa kwenye Jela ya Mpanga, iliopo Kigali, Rwanda, kutumikia adhabu yao. Mahakama ya SCSL, inayoungwa mkono na UM, iliamua kuwapeleka wafungwa hawo wanane Rwanda kwa sababu magereza ya Sierra Leone hayatoshelezi viwango vya sheria ya kimataifa.

Wafungwa wa Sierra Leone ni wafuasi wa makundi ya waasi ya RUF, AFRC na CDF. Miongoni mwa makosa waliotuhumiwa nayo inajumlisha jinai ya kuwageuza mateka wanawake kama watumwa wa kijinsiya, na pia waliendeleza mauaji ya kihorera, na waliwalazimisha watoto wa umri mdogo kushiriki kwenye vita na mapigano. Mahakama ya SCSL ilikubaliana na Serikali ya Rwanda kuwafunga wahalifu wa Sierra Leone kwenye gereza la Mpanga, na moja ya sehemu wafungwa watatumikia adhabu yao ilijengwa siku za nyuma kuwafungia watu waliohukumiwa adhabu na Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR).