Idhaa ya Redio ya UM

Agosti 2009
J J J J A I J
1
2 3 4 5 6 7 8
9 10 11 12 13 14 15
16 17 18 19 20 21 22
23 24 25 26 27 28 29
30 31

Huduma

 12 Agosti 2009
Real Chapisha

Mjumbe wa kwenye 'UM ya Majaribio' anasailia natija za kitaaluma mkutanoni

Mpango wa mazoezi ya kisiasa, unaotambiliwa kama 'Mradi wa UM ya Majribio' hutekelezwa kile mwaka na wanafunzi wa maskuli na vyuo vikuu kadha wa kadha katika dunia. Lengo hasa la mazoezi haya ni kuwapatia wanafunzi wanaoshiriki kwenye mradi, fursa ya kushuhudia hali halisi ya shughuli za UM na taasisi zake mbalimbali, zinazosimamiwa na kuongozwa na raia wa kutoka kila pembe ya dunia.

Mwaka huu, kwa mara ya awali katika historia ya mazoezi haya mradi wa 'UM ya Majribio' au 'UM ya Kuigiza' badala ya kutekelezwa kwenye maskuli na vyuo vikuu ulifanyika katika kumbi za UM yenyewe. Kwa muda wa siku chache, katika mwezi Agosti wanafunzi karibu 500 waliowakilisha vyuo vikuu, kutoka nchi wanachama 70, walishiriki kwenye mazoezi ya 'UM ya Kuigiza' yaliofanyika ndani ya kumbi za Makao Makuu ya Ofisi ya UM iliopo Geneva. Miongoni mwa wanafunzi waliohudhuria kikao alijumuika kijana wa kutoka Tanzania, Samafila Aianan. Patrick Maigua, mwendeshaji vipindi wa Redio ya UM-Geneva alifanya mahiojiano maalumu na mjumbe huyo wa Tanzania.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.