Idhaa ya Redio ya UM

Julai 2009
J J J J A I J
1 2 3 4
5 6 7 8 9 10 11
12 13 14 15 16 17 18
19 20 21 22 23 24 25
26 27 28 29 30 31

Huduma

 9 Julai 2009
Real Chapisha

Hapa na pale

Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jana lilimaliza Mkutano wa Dunia juu ya Iimu ya Juu uliofanyika Paris, ambapo kulitolewa mwito maalumu unaozitaka nchi wanachama kuongeza mchango wao katika juhudi za kukuza ilimu. Kwenye taarifa rasmi ya mkutano, wajumbe waliowakilisha nchi 150 walitilia mkazo umuhimu wa kuwekeza posho ya bajeti lao kwenye sekta ya ilimu, ili kujenga jamii yenye maarifa anuwai, na inayomhusisha kila raia, ambaye atapatiwa fursa sawa ya kushiriki kwenye tafiti za hali ya juu, huduma itakayowakilisha uvumbuzi na ubunifu wenye natija kwa umma.

Mkutano wa Hadhi ya Juu wa Baraza la UM Juu ya Uchumi na Jamii (ECOSOC), ulioanzisha mijadala yake Ijumatatu iliopit mjini Geneva, leo Alkhamisi umehimtimisha kikao chake cha mwaka. Masuala yaliopewa umuhimu kwenye mkutano wa mwaka huu ni yale yanayohusu maamirisho ya afya ya jamii. Wajumbe wa ECOSOC walinasihiwa kutopuuza ahadi walizotoa siku za nyuma kuyasaidia mataifa masikini kukamilisha kwa wakati Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), licha ya kuwa ni kweli ulimwengu umekabiliwa sasa hivi na mizozo kadha ya ya kifedha na uchumi. Waraka wa Maafikiano ya Mkutano umehadharisha kwamba mizozo hiyo inahitajia kudhibitiwa mapema kwa sababu inahatarisha sana kuangamiza yale maendeleo ya MDGs yaliofanikiwa kutekelezwa.

Ijumamosi, tarehe 11 Julai ni Siku ya Udhibiti wa Idadi ya Watu Duniani. Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNFPA) ilieleza kwenye taarifa kwa waandishi habari juu ya siku hiyo kwamba uwekezaji wenye kulenga maendeleo ya wanawake ndio mradi wenye fursa ya kuandaa mazingira imara, yatakayosaidia kufufua uchumi, kupunguza umasikini na kukomesha utovu wa usawa wa kijinsia. Kwa mujibu wa UNFPA afya za wanawake zinajumuisha mchango muhimu wa kiuchumi katika nchi zinazoendelea, ambapo imeoenekana wanawake hujumlisha nusu ya wafanyakazi katika sekta ya kilimo. Kwa mfano, katika bara la Afrika wanawake ndio wenye kuhusika na asilimia 80 ya shughuli za kupandisha mazao makuu, na katika nchi za Asia za Kusini-Mashariki asilimia 90 ya wakulima wa mpunga ni wanawake.