9 Julai 2009
TBD
ITU itashirikiana na Qualcomm kuimarisha mawasiliano ya dharura
09/07/2009
Shirika la UM juu ya Mawasiliano ya Kisasa (ITU) limetangaza kwamba litashirikiana na kampuni ya Qualcomm, inayotumia aina ya kisasa ya mawasiliano ya simu bila waya ili kudhibiti vyema huduma za kihali kwenye maafa.
Madhumuni hasa ya ushirikiano huu ni kuimarisha mawasiliano ya dharura na kusaidia kwenye matayarisho ya kukabiliana na maafa ya kimaumbile, na pia kufarajia umma baada ya maafa kutukia. Kwa mujibu wa taarifa ya ITU teknolojiya ya mawasiliano ya kisasa yasiotumia waya ni lazima kujumuishwa kimataifa kwa makusudio ya kuwawezesha wahudumia misaada ya kihali, ya dharura, kuendeleza shughuli zao za kuokoa watu kwenye mazingira yaliofunikwa na maafa ya kimaumbile, baada ya vyombo vya mawasiliano vya ndani ya nchi kuharibiwa.

