Idhaa ya Redio ya UM

Julai 2009
J J J J A I J
1 2 3 4
5 6 7 8 9 10 11
12 13 14 15 16 17 18
19 20 21 22 23 24 25
26 27 28 29 30 31

Huduma

 9 Julai 2009
Real Chapisha

UM-UA kuanzisha programu ya kufuatilia mtiririko wa vitegauchumi Afrika kuwasaidia wafanyabiashara

UM na Umoja wa Afrika (UA) leo wameanzisha chombo kipya chenye madhumuni ya kusaidia kupanga ratiba ya kufuatilia mtiririko wa vitegauchumi katika Afrika, na kuwapatia wafanyabiashara taarifa thabiti wanazohitajia kufanya maamuzi imara juu ya shughuli zao.

UN

UN

 Utaratibu huu wa kuashiria mwelekeo wa uwekezaji ulibuniwa kwa ushirikiano na Shirika la Kampuni ya Microsoft, na utahudumiwa kwenye intaneti, na utajulikana kama Programu ya Jukwaa la Kufuatilia Uwekezaji. Programu hii itakusanya takwimu na taarifa kuhusu mifumo ya wawekezaji wa kizalendo na wale wa kutoka nje ya nchi, na pia kufafanua "mambo yanayowahamasisha kibiashara, utendaji wao, mawazo walionayo, dhamira na athari za hatua wanazofikiria kuzitekeleza kiiktisadi." Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), lenye makao makuu Vienna, Austria lilijumuika na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwenye mkutano uliofanyika Addis Ababa majuzi kuwasilisha rasmi chombo hiki kipya juu ya tathmini ya uwekezaji, ambapo walikusanyika mawaziri wa serikali, wawakilishi wa mabenki, mawakala wenye kuendeleza shughuli za kutangaza uwekezaji wa Afrika pamoja na wawakilishi wa sekta ya binafsi na wataalamu wa shughuli za viwanda. Utaratibu huu wa kufuatilia uwekezaji Afrika utakuwa unakusanya takwimu mpya mara mbili kila mwaka, shughuli itakayoendelezwa na Shirika la UNIDO katika nchi 20 za Afrika, na utafiti wa awali utaanzishwa rasmi tarehe 23 Julai katika mataifa ya Kenya na Senegal.