Idhaa ya Redio ya UM

Juni 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30

Huduma

 30 Juni 2009
Real Chapisha

Tiba ya majaribio dhidi ya usubi imeanzishwa rasmi katika nchi tatu za Afrika, imeripoti WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuanzisha majaribio ya tiba mpya dhidi ya maambukizi ya maradhi ya usubi, katika mataifa matatu ya Afrika - yakijumlisha Ghana, Liberia na JKK.

Maradhi haya, kwa mujibu wa takwimu za WHO, huathiri watu milioni 100 hasa katika bara la Afrika, na kwenye sehemu ndogo za mabara ya Amerika na katika Yemen. Dawa itakayotumiwa kwenye tiba ya majaribio hujulikana, kwa lugha ya kitaaluma, kama moxidectin, na ni tiba inayofanyiwa majaribio kuchunguza kama ina uwezo wa kuua au kufunga kizazi cha wale funza wapevu wanaosababisha maradhi haya ya macho yenye kuleta upofu, yaani maradhi ya usubi. Maradhi ya usubi hutambuliwa vile vile kama maradhi ya upofu wa mtoni, kwa sababu yule nzi mweusi anayeambukiza maradhi haya huzalisha kwenye maeneo ya mto, unaotiririka na kwenda kwa kasi. Majaribio ya tiba hii yataendelezwa kwenye maeno husika kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ijayo.