Idhaa ya Redio ya UM

Juni 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30

Huduma

 30 Juni 2009
Real Chapisha

Uamuzi wa Tanzania kuongeza muda wa makazi kwa Waburundi wapongezwa na UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limekaribisha uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kuruhusu muda zaidi wa kukaa nchini, kwa baadhi ya wahamiaji wa Burundi 36,000 wanaotaka kurejea makwao, kwa khiyari, kutoka kambi ya Mtabila iliopo wilaya ya Kasulu, kaskazini-magharibi katika Tanzania, kambi ambayo ilipangwa kufungwa mnamo tarehe 30 Juni 2009.

Wahamiaji hawa wa Burundi walikuwa wakiishi Tanzania tangu miaka ya 1990. Kuanzia 2002, UNHCR imefanikiwa kusaidia kuwarejesha makwao, kwa khiyari, wahamiaji wa Burundi 485,000 waliokuwa wakiishi katika  mataifa jirani ya Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda.