Idhaa ya Redio ya UM

Juni 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30

Huduma

 29 Juni 2009
Real Chapisha

Wajumbe wa Kundi la Kazi la UM kwa waliopotezwa na kutoweka wahitimisha kikao cha 88 Rabat

Wajumbe wa Kundi la Kufanya Kazi la UM juu ya Watu Waliolazimishwa Kupotea na Kutoweka baada ya kukukamilisha ziara yao ya siku nne katika Morocco walikutana kwenye mji wa Rabat na kukamilisha kikao cha 88 kilichofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Juni walipozingatia masuala yanayohusika na watu kukamatwa kimabavu na kutoweka wasijulikane walipo.

Tume ilifanya mapitio ya kesi 200 juu ya watu waliotoewka katika mataifa 35. Kadhalika, walitathminia tuhumu zinazoambatana na mashirika yasio ya kiserikali yanayodai kuwepo vizingiti kwenye nchi kadha, vizingiti ambavyo vinakwamisha utekelezaji halali wa Mwito wa Kuhifadhi Watu, mwito unaoharimisha Vitendo vya Kuwatorosha na Kuwapoteza Raia Kimabavu. Vile vile wajumbe wa Kundi la Kufanya Kazi, la UM, wamemteua Jeremy Sarkin, kuwa Mwenyekiti mpya wa tume hiyo kwa miaka miwili ijayo, kuanzia tarehe 1 Agosti 2009.