Idhaa ya Redio ya UM

Juni 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30

Huduma

 29 Juni 2009
Real Chapisha

Mkutano wa UM umepitisha ratiba mpya kupunguza athari za miporomoko ya uchumi duniani

Wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mzozo wa Uchumi na Fedha Duniani na Athari zake kwa Maendeleo, wameafikiana Ijumaa ratiba mpya ya mpango wa utendaji, utakaotumiwa na Mataifa Wanachama kipamoja, kupunguza makali na kasi ya miporomoko ya uchumi katika nchi zinazoendelea.

Maafikiano haya yalijumlishwa kwenye waraka uliokuwa na vifungu 60 utakaotumiwa Baraza Kuu kupitishwa baadaye kwenye kikao cha mwaka huu. Raisi wa Baraza Kuu Miguel d'Escoto Brockmann aliwakumbusha wajumbe wa kimataifa kwamba "jumuiya yote ya kimataifa inahimizwa kuongeza michango ya pamoja ili kusuluhisha mizozo ya kiuchumi na fedha kimataifa kwa mafanikio." Ijumatatu asubuhi Baraza Kuu lilikutana tena ambapo wajumbe wa kimataifa walibadilishana mawazo ziada juu ya suluhu zinazoridhisha, kutumiwa kukabili masuala ya mizozo ya fedha na uchumi, yaliopamba mataifa maskini katika siku za karibuni.