26 Juni 2009
TBD
WTO/UNEP yametoa ripoti inayothibitisha fungamano hakika kati ya biashara na mabadiliko ya hali ya hewa
26/06/2009
Shirika la Biashara Duniani (WTO) na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) yametangaza bia ripoti mpya yenye kuelezea, kwa mara ya kwanza, fungamano ziliopo baina ya biashara ya kimataifa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Ripoti ilisema biashara huru ya kimataifa ni kadhia mojawapo inayosaidia udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa kwa kupunguza umwagaji wa hewa chafu kwenye anga, na kurekibisha hali ya mazingira kwa kufarajia zana za kisasa.

