TBD
Mzozo wa waliong'olewa makazi Usomali waendelea
Vile vile kuhusu Usomali, Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuwa na wasiwasi juu ya athari kwa umma, kuokana na mripuko wa mapigano yaliosababisha mzozo mkubwa wa watu kung'olewa makazi kujiri kwa hivi sasa katika Usomali.
UNHCR ilisema tangu mapigano kuanza - mnamo tarehe 07 Mei (2009) - baina ya vikosi vya serikali na kundi la wapinzani la Hizb al Islam, kwenye sehemu za kaskazini-magharibi ya Mogadishu, raia kadha walijeruhiwa, na uharibifu mkubwa wa eneo ulishuhudiwa kutokana na vurugu hili. Kwa mujibu wa taarifa za hospitali, raia 250 waliuawa na watu 900 walijeruhiwa. UNHCR inakadiria tangu mapigano kuanzishwa watu 160,000 walilazimika kuyahama makazi yao na kuomba hifadhi kwenye sehemu nyengine za Usomali na katika mataifa jirani.

