TBD
Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mzozo wa Fedha Duniani watia kikomo
Mkutano Mkuu juu ya Mzozo wa Uchumi na Fedha Duniani na Athari Zake Kwa Maendeleo umekamilisha majadiliano Ijumaa alasiri.
Kwenye kikao cha Allkhamisi ya jana, wajumbe wa kimataifa walijaribu kusawazisha tofauti zao za kimawazo, kwa madhumuni ya kuleta makubaliano ya jumla, yatakayojumuishwa kwenye waraka wa azimio la Mkutano. Maafikiano haya yakikamilishwa yanatumainiwa kuyasaidia Mataifa Wanachama kuepukana na matatizo ya kiuchumi na kifedha yakiibuka tena katika siku za baadaye. Mpokezi wa Tunzo ya Uchumi ya Nobel, Profesa Joseph Stiglitz wa Chuo Kikuu cha Columbia klichopo New York, Marekani kwenye mahojiano aliokuwa nayo na waandishi habari waliopo Makao Makuu Alkhamisi juu ya maendeleo ya mkutano, alitoa mwito uliopendekeza mataifa yote wanachama katika UM yajumishwe kwenye usanifu wa mfumo mbadala, utakaoongoza shughuli za uchumi na kifedha kwenye soko la dunia. Alisema wakati umewadia kwa walimwengu kubuni mfumo mpya wa kutunza na kuhudumia akiba ya fedha ya kimataifa utakaolingana na mahitaji ya karne ya sasa.

