Idhaa ya Redio ya UM

Juni 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30

Huduma

 25 Juni 2009
Real Chapisha

Mapigano ya kikabila Kenya yamesababisha maelfu ya wakuria kung'olewa makazi

Shirika la UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) limetangaza kupamba hali ya wasiwasi mkuu kwenye wilaya ya Kenya ya Kuria Mashariki, karibu na mpaka na Tanzania, ambapo majuzi watu 6,000 waling'olewa makazi kwa sababu ya mapigano yaliozuka miongoni mwa jamii ya makabila ya Kuria.

James Kisia, naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya Msalaba Mwekundu ya Kenya (KRCS) alisema licha ya kuwa karibuni hawakusajili tukio la mashambulio wala nyumba kuunguzwa moto kwenye wilaya hiyo, hali ya wasiwasi bado ilionekana kuendelea kujizatiti kieneo. Mapigano baina ya makundi yenye asili za Ki-Nyabasi na Ki-Buirege, ambazo ni miongoni mwa makabila ya jamii ya Kikuria, yalianzishwa mnamo mwisho wa mwezi Mei, kufuatia tukio la wizi wa ng'ombe ambapo iliripotiwa watu wawili waliuawa. Shambulio la kulipa kisasi, liliofuatia baada ya hapo, nalo lilisababisha tena vifo viwili ziada na nyumba kadha zilichomwa moto. Tawi la Ofisi ya OCHA Kenya, pamoja na mashirika yanayohudumia misaada ya kiutu, yamejumuika kipamoja sasa hivi nchini kuandaa shughuli za kufarajia misaada ya kihali kwa umma uliong'olewa makazi, kwenye wilaya ya Kuria Mashariki.