Idhaa ya Redio ya UM

Juni 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30

Huduma

 25 Juni 2009
Real Chapisha

Wataalamu wa UM wamehadharisha wajumbe wa Kikao cha BK juu ya Mzozo wa Uchumi kutosahau kufungamanisha haki za binadamu kwenye maamuzi yao

Magdalena Sepúlveda na Cephas Lumina, Wataalamu Huru wawili wa UM wanaohusika na masuala ya haki za kibinadamu kwenye mazingira ya umaskini uliovuka mipaka na kuhusu athari haribifu za madeni, wametuma taarifa maalumu kwenye Mkutano wa Baraza Kuu juu ya Mizozo ya Uchumi na Kifedha, iliohimiza Mataifa Wanachama "kuchukua hatua za dharura, zitakazosaidia kuendeleza ufufuaji wa muda mrefu wa shughuli za kiuchumi na fedha, kwa kutunza haki za kimsingi kwa umma mamskini wenye kusumbuliwa zaidi na matatizo haya ya kiuchumi" kwa kupatiwa huduma za jamii.

Walionya kwamba pindi halaiki ya raia wasiojiweza, na wasio na kazi, wataendelea kunyimwa msaada wa serikali kumudu maisha wastani ya kikawaida, mamilioni yao watajikuta kunaswa tena kwenye mkondo wa ufukara na hali duni ya muda mrefu. Walilihimiza Baraza Kuu la UM kutumia utekelezaji wa haki za binadamu kuwa ndio kigezo cha kutathminia uwajibikaji wa Taifa kuhudumia mahitaji ya umma dhidi ya usumbufu unaoletwa na matatizo ya kiuchumi na kifedha, kimataifa hivi karibuni.