Idhaa ya Redio ya UM

Juni 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30

Huduma

 25 Juni 2009
Real Chapisha

Hapa na pale

Tume ya Umoja wa Afrika (UA) kwa Darfur, inayoongozwa na Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki imeripotiwa kukamilisha vikao vya siku 10, kusikiliza kauli za umma, ili kutafuta njia za kuharakisha suluhu ya mpango wa amani katika Darfur na kuandaa mazingira ya kuleta upatanishi miongoni mwa makundi yanayohasimiana na pia haki katika Darfur. Wajumbe wa Tume walikutana na wawakilishi wa vyama vya kisiasa, jumuiya za kiraia, makundi ya waasi, makundi ya kikabila na pia makundi ya wahamiaji wa ndani waliong'olewa makazi katika Khartoum na kutoka miji sita ya jimbo la Darfur. Taarifa hii ilitolewa na Shirika la Mchanganyiko la UM-UA kwa Darfur (UNAMID).

Makao Makuu

Makao Makuu

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti mnamo siku tano zilizopita watu 26,000 waling'olewa makazi kutoka mji mkuu wa Usomali, Mogadishu kufuatia mapigano makali baina ya vikosi vya serikali na wapiganaji wafuasi wa vyama vya KiIslam. Kwa mujibu wa takwimu za UNHCR kuanzia mwanzo wa mwezi Mei, raia 160,000 waling'olewa makazi kwa sababu ya mapigano. UNHCR imeeleza ya kuwa kuharibika kwa hali ya usalama katika mji wa Mogadishu, ni hali inayotatanisha juhudi za mashirika yanayohudumia misaada ya kihali na kuwafunga kikazi, kwa sababu ya usalama ulioregarega na ugumu wa kuwafikia wale raia muhitaji walioathirika na mapigano.

Mashirika 20 ya UM yametuma mwito maalumu kwenye Mkutano wa Mizozo ya Uchumi na Kifedha na Athari Zake dhidi ya Maendeleo, unaofanyika kwenye Makao Makuu, unaoyataka Mataifa Wanachama kurekibisha uchumi wao, kwa kuhakikisha yanatumia utaratibu utakaosaidia kupunguza hewa chafu inayomwagwa katika anga, na kuimarisha uchumi utakaohifadhi kutunza mazingira na kuzalisha fursa za ajira zitakazokuza uchumi, jamii na hifadhi bora kwa mazingira. Taarifa ya mashirika 21 ya UM iliwasilishwa mkutanoni na Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) ambaye alisisitiza mwito wao unamaanisha bidii ya taasisi za UM kuwa mawakala wa kuleta mageuzi yatakayodumisha maendeleo katika karne ya 21.