Idhaa ya Redio ya UM

Juni 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30

Huduma

 23 Juni 2009
Real Chapisha

UNHCR ina wasiwasi na kunyanyuka kihadhi kwa vyama baguzi vipingavyo wageni katika EU

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limetoa mwito maalumu wenye kuisihi Serikali ya Sweden kutumia wadhifa uliokabidhiwa nao sasa hivi, wa uraisi wa Umoja wa Ulaya (EU), kutilia mkazo umuhimu wa nchi wanachama kusimamia shughuli za mipaka yao, kwa kuzitekeleza kanuni za huruma za kuruhusu wahamaji wa kigeni kupata hifadhi, kama ilivyoidhinishwa na haki za kimsingi za kiutu.

UNHCR ilisema matukio ya siku za karibuni, katika mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya, dhidi ya wahamiaji, yameutia wasiwasi mkuu jumuiya ya kimataifa; mathalan, uamuzi wa serikali ya Utaliana kuwarudisha walipotoka, wale wahamiaji waliojaribu kuingia nchini humo kwa mashua, ili kuomba hifadhi ya kisiasa, pamoja na lile tukio la kusikitisha ambapo vyama vya kisiasa vya nchi kadha wanachama wa EU, vyenye sera za kupinga wahamiaji wa kigeni kuingia nchini mwao, vilipata ushindi mkubwa kwenye kura ya karibuni ya Umoja wa Ulaya. Maamuzi haya, kwa mujibu wa UNHCR, yanaonyesha nchi za Umoja wa Ulaya bado zinaregrega kwenye utekelezaji wa ahadi za kuwapatia wahamaji wanaokimbia makwao mateso, na madhila, hifadhi kinga, kwa kulingana na kanuni za kimataifa.