TBD
FAO inasema mamilioni ya hekta za savana Afrika zipo tayari kuvuna natija kuu za kibiashara ya kilimo
Ijumatatu Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza kwamba sehemu kubwa ya ardhi ya savanna, iliotanda katika mataifa 25 barani Afrika, pindi itadhibitiwa na shughuli za kiuchumi kama inavyostahiki, itamudu kuzalisha bidhaa za chakula, kwa wingi kabisa, hali ambayo italiingiza eneo miongoni mwa maeneo yatakayoongoza biashara ya bidhaa za kilimo kwenye soko la kimataifa.
Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na FAO, ikishirikiana na Benki Kuu ya Dunia, juu ya kadhia hiyo, iligundulikana kwamba ni asilimia 10 tu ya ardhi ya savanna, kwenye eneo husika hutumiwa kwa kilimo. Eneo hili muhimu, linalojulikana kama 'ukanda wa Savana wa Guinea,' hujumlisha hekta milioni 400 ya ardhi, sehemu ambayo imetanda kutoka taifa la Senegal, Afrika Magharibi mpaka Afrika ya Kusini.

