Idhaa ya Redio ya UM

Juni 2009
J J J J A I J
1 2 3 4 5 6
7 8 9 10 11 12 13
14 15 16 17 18 19 20
21 22 23 24 25 26 27
28 29 30

Huduma

 22 Juni 2009
Real Chapisha

Ripoti ya kisayansi kuonya walimwengu, mabadiliko ya hali ya hewa duniani sio mzaha

Wataalamu wa kimataifa wa katika fani ya sayansi, juzi waliwasilisha ripoti mpya yenye kusisitiza kwamba mabadiliko ya hali ya hewa, yalioripotiwa kujiri kimataifa katika miaka ya karibuni, ni matukio hakika kwenye mazingira na sio mnong'ono wala makisio.

Ripoti hii yenye kurasa 36 imetahadharisha, "ulimwengu sasa hivi unakabiliwa na mkondo wa hatari inayokithiri, ya kuzuka kwa mabadiliko ya ghafla, na yasiorudishika nyuma, ya hali ya hewa" ambayo ni wajibu kudhibitiwa haraka, kabla hayajasambaza madhara yake kimataifa. Ripoti ilijumuisha mukhtasari wa matokeo ya tafiti 1,400 ziada, zilizowakilishwa kwenye mkutano mkuu wa mwezi Machi 2008, uliofanyika katika mji wa Copenhagen, uliohudhuriwa na wanasayansi 2,000 kutoka nchi 70, ambao kwenye taarifa zao walisisitiza, kwa kauli moja, ya kuwa ushahidi mpya waliokusanya ulithibitisha kihakika mabadiliko ya hali ya hewa duniani yanatukia kwa kasi, hivi sasa, kukiuka kile kiwango kilichoashiriwa maka miwili iliopita. Walisema majabali ya barafu kwenye bahari ya Aktiki (Arctic) yanaendelea kuyeyuka na kusababisha vina vya maji kunyanyuka kutoka uketo wa bahari, na hali ya hewa ilokiuka mipaka inazuka pia katika sehemu mbalimbali za dunia, nje ya majira ya kikawaida, na halijoto pia nao kwenye bahari kuu imebainika kukithiri kwa kima kikubwa, na wakati huo huo gesi za sumu zilizonaswa na kufunikwa na utando wa theluji kwa maelfu ya miaka, sasa zimeonekana vile vile kuanza kuvuja na kuchafua angahewa. Ripoti ya wanaasayansi imetia mkazo ya kuwa upunguzaji wa dharura, na wa mapema wa hewa chafu inayomwaga angani, ndio kadhia muhimu inayotakikana kuendelezwa sasa hivi na yenye uwezo wa kuteremsha kasi ya muongezeko wa halijoto kwenye mazingira ya kimataifa.