25 Machi 2009
TBD
Mahojiano na Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya Hassan Omar
25/03/2009
Muasisi wa kundi la kutetea Haki za Binadamu "Oscar Foundation", Oscar Kamau Kingara aliuliwa pamoja na mshauri wake wa habari John Paul Oulu wakiwa garini karibu na chuo kikuu cha Nairobi.
Walikuwa wakielekea kwenye mkutano na maafisa wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Kenya, Alhamisi 5 Marchi 2009. Abdushakur Aboud alizungumza na Bw Hassan Omar, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya KNCHR, akisema wamelaani mauaji hayo ya kikatili na kutaka uchunguzi kamili ufanyike.

