Idhaa ya Redio ya UM

Kuunganisha

Huduma

Lugha zinazotangazwa kwenye Radio ya UM

Radio ya Umoja wa Mataifa inatangza habari kila siku kwa lugha ya Kiswahili, Kiarabu, Kichina, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kirusi na Kihispania. Na mara moja kwa wiki inakuwa na vipindi vya lugha ya French Creole, Kibengal, Kihindi, Urdu na kiindonesia.

Radio ya UM inabadilisha taarifa zake kutokan na habari mpya zinavyokuja kila mara kwa siku. Pia inaandaa makala na kufanya uchambuzi wa mada mbalimbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi, maendeleo na masuala yanayohusu tamaduni yanyohusisha Umoja wa Mataifa na kazi zake. Vipindi vya Radio ya Um viko vingi ni kuanzia habari binafsi, makala, vipindi maalumu na taarifa za habari za kila siku na zile za kila wiki.

Na vipindi vyote hivyo vinaweza kutumiwa na vyombo vingine vya habari au watangazaji, na vinaweza kutumiwa kama chanzo cha habari kwa waandishi binafsi.Na kwa kuongezea tuu ni kwamba vipindi vyote hivyo na sauti zingine kwenye tovuti yetu vinatolewa bure bila malipo yoyote

Kwa uchaguzi zaidi wa ushirikiano usisite kuwasilina nasi. contact us.