Miili ya walinda amani wa Tanzania waliouawa DRC yawasili Dar es salaam

Kusikiliza /

 

Milingoti ya bendera za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwa bila bendera hii leo ikiwa ni kuomboleza mauaji ya askari wa Tanzania waliouawa wakilinda amani chini ya Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. (Picha:UN/Idhaa ya Kiswahili/Leah Mushi)

Miili ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa  14 waliouawa katika mashambulizi huko kivu ya kaskazini, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongpo-DRC mwishoni mwa wiki iliyopita  imewasili nchini Tanzania leo  kwa ajili ya mipango ya mazishi. Lean Mushi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Leah Mushi)
Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York nchini Marekani, bendera za nchi wanachama 193 hazijapandishwa katika milingoti hii leo na ya Umoja wa Mataifa ikipepea nusu mlingoti.
Hii ni ishara ya maombolezo ya  walinda amani hao kutoka Tanzania waliouawa na wengine 53 kujeruhiwa nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
Nimezungumza na Sylvia Mpanda dada wa mmoja wa marehemu  Private Deogratius Kamili nikitaka kufahamu nini kinaaendelea kwenye ngazi ya familia
(Mahojiano)

Miili ya walinda amani  wa Tanzania waliouawa wakati wa mapigano huko Semuliki, jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hapa ni Beni wakati wa kuaga miili hiyo ambayo tayari wamewasili Dar es salaam. (Picha:MONUSCO)

Tayari Umoja wa Mataifa likiwemo Baraza la usalama la wamelaani vikali mauaji hayo na kusema kuwa yanafifisha juhudi za kutafuta suluhu katika jamuhuri ya kidemokrasia Kongo DRC.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031