Mbinu za kupunguza njaa zazaa matunda Nigeria

Kusikiliza /

Wakulima Nigeria wajivunia mazao(Mtama)ya shamba lao.Picha: FAO

Hiki kitakuwa chakula chakunitosha mimi na familia yangu na kingine nitauza na pesa nitatumia kuwapeleka watoto shule.

Hii ni kauli ya leo Aisha Ibrahim ambayo haikuwahi kusikika kwa miaka 3 iliyopita lakini leo Aisha anaisema baada ya kuvuna mazao yake huko Yobe nchini Nigeria.

Baadhi ya mbegu yaliyosambazwa na FAO kusaidia wakulima wakimbizi. Picha: FAO

Shukrani wakizitoa kwa shirika la Chakula Kilimo la Umoja wa mataifa FAO pamoja na washirkia wake waliowapatia mbegu bora za mazao na mbolea pamoja na mbinu bora za kilimo.

Yobe ni moja kati ya maeneo yaliyoathiriwa na mashambulizi ya Boko Haramu lakini baada ya waasi hao kuondoka na wananchi kusaidiwa kurejea katika makazi yao na kupatiwa misaada mbalimbali maisha yameanza kurejea kawaida.

Ripoti zinaonesha kupungua kwa njaa Nigeria. Picha: FAO

Ripoti zinaonesha kupungua kwa njaa kwenye maeneo yaliyokuwa na vita ambapo sasa idadi ya watu wenye njaa imepungua kutoka watu Milioni 5.2 hadi milioni 2.6 kwa kipindi cha miezi mitatu pekee

Ripoti ya awali ya kiwango cha njaa Nigeria. Picha: FAO

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031