Matrilioni ya dola yatumika kwa rushwa duniani:UNDP

Kusikiliza /

Picha ikionyesha jinsi rushwa inavyotolewa . Picha hiyo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP katika siku ya kimataifa ya kupinga rushwa.

Kiwango cha kila mwaka cha rushwa duniani kinakadiriwa kuwa dola ya trilioni moja, wakati huo huo uchumi wa dunia unapoteza dola trilioni 2.6 kutokana na rushwa.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP , katika nchi zinazoendelea hasarara zinazohusiana na ufisadi au rushwa zinazidi mara 10 msaada rasmi wa maendeleo.

Katika siku ya kimataifa ya kupinga ufisadi inayoadhimishwa kila mwaka Desemba 9, Umoja wa Mataifa umekumbusha kwamba rushwa ni uhalifu mkubwa ambao unaathiri maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika taifa lolote, na kuongeza kuwa hakuna nchi, wala kanda ambayo ina kinga dhidi ya rushwa.

 

Mwaka huu ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uhalifu na madawa UNODC na shirika la UNDP wameanzisha kampeni ya pamoja yenye lengo la kuelewa ni jinsi gani rushwa inaathiri elimu, afya, haki na demokrasia.

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031