Machafuko mapya, misaada ya kibinadamu zaidi yahitajika YEMEN

Kusikiliza /

Mfanyakazi wa UNHCR akishauriana na viongozi wa wazee na kijamii kwenye eneo la Dharawan lililoko kwenye viunga vya mji mkuu wa Yemen, Sana’a.
© UNHCR/Shabia Mantoo

Machafuko mapya yameibuka magharibi mwa pwani ya Yemen na kusababisha watu kuyakimbia makazi yao

Zaidi ya watu 1,400 wamekimbilia majimbo ya Taizz na Hudaydah na kwenda maeneo mengine ambako huko wanahitaji misaada ya kibinadamu

Msemaji wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Babar Baloch amesema kuwa tayari misaada ya dharura imepelekwa kwa zaidi ya familia 2000 huko Hudaydah.

Hata hivyo kwa kuwa bandari ya Hudaydah imefungwa, wameshindwa kuwasilisha vifaa kama vile vile banketi,  vyakula na dawa vilivyomo kwenye kontena 43 bandarini humo.

UNHCR imeziomba mamlaka za Yemen kuharakisha utoaji wa mizigo hiyo kwa kuwa inahitajika sana na kuna bidhaa zinazoharibika mapema kama vile dawa.

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031