Nyumbani » 14/12/2017 Entries posted on “Disemba 14th, 2017”

Magonjwa ya msimu yagharimu maisha ya zaidi ya watu 650,000

Kusikiliza / Picha ya shirika la afya ulimwenguni  ikionyesha mtu mwenye  magonjwa ya njia ya hewa

Ripoti mpya ya Shirika la afya duniani WHO na kituo cha kudhibiti wa magonjwa cha Marekani, CDC,  imesema  zaidi vifo 650,000 kila mwaka vinahusishwa na magonjwa ya njia ya hewa ikiwemo homa ya mafua inayoambukiza watu nyakati tofauti za misimu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna ongezeko kubwa kutoka idadi ya vifo kati ya 250,000  [...]

14/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kituo cha kupima TB Kibong'oto kuleta nuru kwa wachimbaji madini

Kusikiliza / PICHA: Waziri wa Afya nchini Tanzania Ummie Mwalimu akizindua kituo hicho. Picha: Kwa hisani ya NLTP-TZ

Vumbi vumbi wanalokumbana nalo wachimba madini wadogo limeendelea kuwa mwiba katika afya zao. Nchini Tanzania hususan mkoani Manyara, ushuhuda wa mmoja wa wachimbaji wadogo umeonyesha dhahiri shairi kuwa hatua ni lazima zichukuliwe ili kuepusha nguvu kazi hiyo dhidi ya ugonjwa wa Kifu Kikuu au TB ambao ingawa una tiba bado unaleta kadhia. Ukosefu wa vituo [...]

14/12/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Seneti Mexico msipitishe muswada wa sheria Mexico: Wataalam

Kusikiliza / UNHRC-Logo

Muswada wa sheria mpya unaolenga kuvipatia vikosi vya ulinzi nchini Mexico kujikita na kazi za polisi bila  kuwajibika kwa jamii unatia shaka kuhusu haki za binadamu Hayo yamesemwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu hii leo huko Geneva Uswisi. Wataalamu hao wamesema muswada huo unaotarajiwa kupitishwa leo na baraza la seneti nchini humo, unatakiwa kupingwa kwa kuzingatia [...]

14/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hotel iza Phuket zachukua hatua kuhifadhi baharí

Kusikiliza / Kampeni ya #Cleanseas. Picha: UNEP

Shirika la umoja wa matafa la mazingira UNEP limekaribisha jitihada za muungano wa hoteli za kifahari za Phuket nchini Thailand pamoja na maduka mengine makubwa kwenye ukanda huo za kujitolea katika kampeni ya  usafi wa bahari. Anthony Lark ambaye ni mwenyekiti wa muungano huo unajumuisha hoteli za kifahari kama JW marriot, Hyatt, Hilton Novotel, swissotel [...]

14/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Buriani!

Kusikiliza / Kwaheri

Leo imekuwa ni siku ya huzuni na majonzi makubwa nchini Tanzania ambako serikali, jeshi na wananchi na Umoja wa mataifa wamejumuika jijini Dar es salaam kuwaenzi na kuwapa mkono wa kwaheri mashujaa 14 walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka nchini humo waliouawa katika shambulio la wiki iliyopita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC [...]

14/12/2017 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Serikali wekeza dola 1 katika afya upate dola 20 za mapato- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kulia) huko Tokyo, Japan akihutubia jukwaa la afya kwa wote. Picha: UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko Tokyo nchini Japan ambako amekuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hizo Shinzo Abe. Katika mkutano wao na waandishi wa habari, Bwana Guterres ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya usalama kwenye rasi ya Korea. Amesema kila mtu anataka kuepusha hali isiwe mbaya zaidi na kwamba [...]

14/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kweli nyumbani ni nyumbani: UNHCR

Kusikiliza / Binti Fadumo , akiwa kwenye biashara yake ya kuuza batiki mjini Kisimayo Somalia. Amerejea nyumbani na kuanza maisha mapya kwa msaada wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR  baada ya kuishi ukimbizi kambini Dadaab nchini Kenya kwa miaka mingi. Picha na UNHCR

Wahenga walinena msahau kwao mtumwa, na nyumbani ni nyumbani hata iweje. Kauli hiyo si msemo tena bali ni hali halisi kwa maelfu ya wakimbizi wa Kisomali walioamua kuchukua hatua ya kurejea nyumbani baada ya kuishi kwa miaka mingi kwenye makambi ya wakimbizi ya Dadaab na Kakuma nchini Kenya. Flora Nducha na taarifa kamili. Natts…… Kisimayu [...]

14/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031