Nyumbani » 13/12/2017 Entries posted on “Disemba 13th, 2017”

Lacroix awajulia hali majeruhi wa Tanzania waliolazwa Uganda

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix awajulia hali walinda amani wawili wa Tanzania waliolazwa katika hospital ya Mulago mjini Kampala nchini Uganda. Picha: UM

Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amewajulia hali walinda amani wawili wa Tanzania waliolazwa katika hospital ya Mulago mjini Kampala nchini Uganda. Walinda amani hao wanapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa wakati wa shambulio huko Semuliki, Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Alhamisi ya wiki iliyopita. Akiwa wodini [...]

13/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za afya zakomba mifuko ya watu- Ripoti

Kusikiliza / Nusu ya idadi ya watu duniani bado wanakabiliwa na ukosefu wa huduma muhimu ya bima ya  afya. Picha: World Bank

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema nusu ya idadi ya watu duniani hawapati huduma muhimu za afya huku wakitumia asilimia 10 ya mapatao yao kusaka huduma hizo na hivyo kutumbukia kwenye umaskini. Taarifa zaidi na Selina Jerobon. (Taarifa ya Selina Jerobon) Takwimu hizo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo huko Tokyo, Jaopan na [...]

13/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

AU yakanusha madai ya ukiukaji wa haki za binadamu Somalia

AU Logo. Picha: AMISOM

  Tume ya muungano wa Afrika imekanusha madai ya ukiukaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na vikosi vyake vya kulinda amani nchini Somalia AMISOM, madai yaliyopo katika ripoti ya pamoja iliyozinduliwa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na na kundi la ulinzi [...]

13/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yajenga uwezo polisi kuelekea uchaguzi mkuu DRC

Kusikiliza / Wapiga kura DRC(maktaba). Picha: MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO unaendesha mafunzo ya kujengea uwezo wasimamizi wa uchaguzi pamoja na polisi nchini humo wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwakani. Mkuu wa kitengo cha polisi, MONUSCO Kamishna Mkuu Awalé Abdounasir, amesema mafunzo hayo yanayofanyika kwenye mji mkuu Kinshasa, yanalenga kuhakikisha polisi wanazingatia [...]

13/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola bilioni 1.7 zahitajika kusaidia wananchi wa Sudan Kusini

Kusikiliza / Mtoto mkimbizi wa Sudan Kusini.(Picha:UNMISS)

Mzozo nchini Sudan Kusini ukiingia mwaka wa nne, zaidi ya dola bilioni 1.7 zahitajika ili kukidhi mahitaji ya kibinadamu kwa nchini humo kwa mwaka 2018. Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini humo Alain Noudéhou ametangaza kiwango hicho hii leo kwenye mji mkuu, Juba akisema mpango huo unalenga watu milioni 6 walioathiriwa [...]

13/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taka za kielektroniki zasalia kwenye makabati majumbani- Ripoti

Kusikiliza / Taka ngumu2

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini ongezeko kubwa la taka za kielektroniki ulimwenguni. Taka hizo ni pamoja na betri chakavu, plagi za umeme, majokofu, simu za kiganjani na kompyuta ambazo kiwango chake mwaka 2016 kilifikia tani za ujazo milioni 44.7. Kiwango hicho ni ongezeko kwa asilimia 8 ikilinganishwa na mwaka jana na mwelekeo ni [...]

13/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031