Nyumbani » 12/12/2017 Entries posted on “Disemba 12th, 2017”

Ukimpa mwanamke fursa, jamii itanufaika

Kusikiliza / Mjane aliyepitia madhila mengi kufuatia kifo cha mumewe, Magdalena Mbiya Namutebi. Picha: John Kibego

Kuna usemi wa kwamba ukimuelimisha mwanamke umeielimisha jamii na ukielimisha  jamii basi utakua umeokoa  kizazi cha baadaye. Huu usemi  hauna maana ya upendeleo bali  ni ukweli kwamba ukimpa mwanamke fursa basi  jamii itanufaika zaidi. Hii inatokana na mapenzi, malezi, na moyo wa ujasiri aliojaliwa  mwanamke. Kwamaniki hiyo tunao mfano ya Bi Magdalena Namutebi mwanamke shupavu [...]

12/12/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza laridhia disemba 12 kuwa siku ya upatikanaji kwa huduma za afya

Kusikiliza / Virachai

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limeridhia tarehe 12 mwezi disemba kila mwaka kuwa siku ya upatikanaji wa afya kwa watu wote duniani. Wajumbe wa baraza hilo wamefikia hatua hiyo baada ya kupitisha azimio nambari A/72/L.27 ambalo likipatiwa jina upatikanaji huduma kwa afya ya wote na liliwasilishwa na mwakilishi wa kudumu wa Thailand kwenye [...]

12/12/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Fedha sio tatizo kasi ya hatua zetu ndio tatizo : Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano wa

Viongozi wa dunia leo wamekusanyika mjini Paris Ufaransa wakijaribu kusaka fedha zaidi ili kuusukuma uchumi wa dunia kuwa unaojali mazingira ikiwa ni miaka miwli kamili tangu kutiwa saini kwa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tambia nchi kuepuka zahma kubwa zaidi ya ongezeko la joto duniani. Akizungumza katika mkutano huo  wa "dunia moja" , Katibu [...]

12/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhila dhidi ya raia yaongezeka mzozoni Ukraine; UM

Kusikiliza / Waathirka wa vita vinavyoendelea Ukraine Mashariki. Picha: IOM/UN/Volodymyr Shuvayev

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo inasema madhila dhidi ya raia katika mzozo wa kivita nchini Ukraine huenda yakaongezeka zaidi, kufuatia kuibika upya kwa mapigano. Ripoti hiyo inasema mapigano hayo yameathiri watu milioni nne nukta nne kwa sasa, yakisababisha vifo zaidi na uharibifu mpya kwa miundombinu muhimu ya maji inayohifadhi kemikali hatari, kinachotishia uhai wa [...]

12/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuondoka kwa kaka, familia imepoteza dira- Yasir

Kusikiliza / Miili ya walinda amani wa UM yafikishwa Tanzania. Picha: UM

Nchini Tanzania uchunguzi wa miili ya walinda amani waliouawa kwenye shambulizi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC unaendelea wakati huu ambapo wafiwa nao wamezungumzia vile ambavyo wamepokea msiba huo. Kwa mujibu wa afisa wa habari wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, UNIC, Stella Vuzo, uchunguzi wa miili hiyo 14 unafanyika [...]

12/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Djibouti yafuata nyayo kuwakumbatia wakimbizi, UNHCR yakaribisha

Kusikiliza / Watoto wakimbizi kutoka Yemen wanaoishi katika kituo cha muda kwenye nyumba ya watoto yatima ya Al-Rahma huko Obock. Picha: © UNHCR / Marie-Claire Sowinetz

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekaribisha  kwa furaha sheria mpya iliyopitishwa nchini Djibouti inayowapatia wakimbizi walioko nchini humo fursa ya  kupata huduma za msingi za kijamii bila vikwazo. Assumpta Massoi na taarifa kamili (TAARIFA YA ASSUMPTA MASSOI) Kwa mujibu wa UNHCR, sheria hiyo mpya inayowapa wakimbizi nafasi ya kupata elimukuingia katika [...]

12/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wapatao 400,000 wakabiliwa na utapiamlo kasai DRC: UNICEF

Kusikiliza / UNICEF kukabiliana na changamoto ya utapiamlo kwa kinamama na watoto nchini DRC. Picha: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF,  limesema zaidi ya watoto 400,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano huko  eneo la Kasai nchini jamhuri ya kidemokrasia la Congo, DRC,  wanakabiliwa na utapiamlo  uliokithiri . Mwakilishi wa UNICEF nchini DRC,  Dkt. Tajudeen Oyewale amesema matatizo ya lishe kwa  watoto hao yamesababishwa na migogoro nchini humo, hivyo kufanya [...]

12/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya chanjo kwa watoto wa Rohingya yaanza :UNICEF/WHO

Kusikiliza / Msichana mdogo anabeba mtoto mgonjwa kwenye Kituo cha Matibabu cha Jeshi katika Kambi ya Wakimbizi ya Kutupalong, Makazi ya muda. Picha: OCHA / Anthony Burke

Serikali ya Bangladeshi kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, shirika la afya duniani WHO na muungano wa chanjo GAVI, leo wamezindua kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa dondakoo na magonjwa mengine yanayozuilika kwa watoto wote wakimbizi wa Rohngya walio na umri wa kati ya wiki sita hadi miaka [...]

12/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 75 zahitajika kusaidia wakimbizi DRC

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani DRC. Picha: IOM

Shirika uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limeomba dola milioni 75 kwa ajili ya kusaidia watu wanaokimbia makazi yao sababu ya machafuko nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC. Tamko hilo linafuatia ziara ya mkurugenzi wa uendeshaji na dharura wa IOM Mohamed Abdiker nchini DRC ambako amesema uwepo wa machafuko maeneo mengi duniani umelifanya eneo [...]

12/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuwekeza kwenye Malaria ni hatua chanya- Dkt. Winnie

Kusikiliza / Mama akiweka neti nchini Tanzania.(Picha:WHO S. Hollyman)

Uwekezaji katika kukabiliana na Malaria, ni uwekezaji ambao utasaidia siyo tu kutokomeza umaskini bali pia kuchochea maendeleo kwa ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla. Dkt. Winnie Mpanju Shumbusho, ambaye ni mwenyekiti wa ubia wa kutokomeza Malaria duniani, RBM amesema hayo katika mahojiano maalum na Idhaa hii akisema kuwa.. (Sauti ya Dkt. Winnie Mpanju Shumbusho) [...]

12/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031