Nyumbani » 06/12/2017 Entries posted on “Disemba 6th, 2017”

Hakuna mbadala wa kuwa na mataifa mawili Mashariki ya Kati:Guterres

Kusikiliza / Antonio Guterres na waandishi wa habari

“Nitafanya kila niwezalo ndani ya uwezo wangu kuunga mkono viongozi wa Israel na Palestina kurejea katika meza ya majadiliano na kutambua mtazamo wa kuwa na amani ya kudumu kwa watu wa pande zote mbili.” Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao [...]

06/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Aibu ya mshtakiwa ni aibu yake na si jamii – ICTY

Kusikiliza / Mwendesha Mashtaka wa ICTY2

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya uhalifu wa kimbari katika iliyokuwa Yugoslavia, ICTY, Serge Brammetz ametaja kile kinachopaswa kufanyika ili kuleta maridhiano kamili kutokana na uhalifu uliotokea kwenye eneo hilo. Amesema hayo akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kufuatia madai ya baadhi ya watu ya kwamba mahakama hiyo bado haijafanikiwa [...]

06/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu huru wa UM kuzuru Korea Kaskazini

Kusikiliza / Mjumbe maaalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Korea kaskazini Tomás Ojea Quintana. Picha: UM/Jean-Marc Ferré

Mtaalamu maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Korea Kaskazini Tomás Ojea Quintana  atakuwa na ziara maalum ukanda wa Asia kukusanya taarifa kuhusu maendeleo katika masuala ya haki za binadamu. Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema ataanzia Korea Kaskazini tarehe 11 hadi 14 mwezi huu na [...]

06/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtembea bure si sawa na mkaa bure- Millard Ayo

Kusikiliza / Millard Ayo akivinjari New  York, Marekani baada ya kutembelea Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. (Picha:Idhaa ya Kiswahili/Patrick Newman)

Vijana ni nguvu kazi inayotegemewa katika kuboresha mustakabali wa dunia. Hata hivyo suala la  ajira limekuwa ni tatizo kubwa miongoni mwa kundi hilo katika maeneo mbalimbali duniani. Yaelezwa kuwa idadi kubwa ya vijana wanapomaliza shule huishia kufanya kazi zisizokuwa na tija katika maisha yao ilhali wanaweza kupata fursa an  ujuzi kwa njia tofauti na kuboresha maisha yao kama [...]

06/12/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wanaume wa Syria wanalawitiwa na kunyanyaswa :UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wanaume wa Syria wanabakwa na kunyanyaswa kingono. Picha: © UNHCR/Dominic Nahr

Utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR umebaini kwamba ulawiti, mateso na unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanaume na wavulana huenda ni mkubwa zaidi ndani na nje ya Syria kulivyo ilivyodhaniwa hapo awali. Waathirika wameeelezea madhila yanayowasimu hususani mahabusu ikiwemo kuvuliwa nguo zote na kuachwa utupu, kuwekwa kizani usiku kucha, [...]

06/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afrika Kusini yachomoza kwenye usajili wa hataza ugenini

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Francis Gurry (kushoto) na Mkuu wa wizara ya Fedha Carsten Fink wazungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Ripoti ya Viashiria vya Mali ya Ulimwengu. (Picha: WIPO / Berrod).

Afrika Kusini imechomoza katika kuwasilisha maombi ugenini ya kusajili hati ya kisheria ili kuepusha kuigwa na watu wengine au hataza. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la hakimiliki la Umoja wa Mataifa, WIPO iliyotolewa leo huko Geneva, Uswisi ikiangazia viashiria vya hakimiliki duniani kwa mwaka 2016. Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Francis Gurry [...]

06/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto milioni 17 wanavuta hewa yenye sumu duniani:UNICEF

Kusikiliza / Mtoto mchanga. Picha: UNICEF

Takribani watoto milioni 17 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja wanaishi katika maeneo ambayo hewa chafuzi ni mara sita zaidi ya kiwango cha juu cha kimataifa na kuwasababisha kuvuta hewa yenye sumu ambayo huweka maendeleo ya ubongo wao hatarini. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto [...]

06/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uganda tokomeza ndoa za utotoni upate dola bilioni 3 kwa mwaka

Kusikiliza / Msichana Aziza, mwenye umri wa miaka 17 akiwa na mimba ya miezi tisa. Picha: UNFPA Tanzania

Ripoti mpya ya Bendi ya Dunia imebaini kuwa iwapo Uganda itatokomeza ndoa za utotoni ifikapo mwaka 2030, basi itakuwa inajipatia faida ya dola bilioni 3 kwa mwaka. Kinyume cha hapo, ripoti hiyo inasema Uganda itashuhudia kushuka kwa elimu miongoni mwa watoto wa Kike, ongezeko la idadi ya watu sambamba na athari za kiafya pamoja na [...]

06/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukusanyaji mapato kuwezesha Somalia kubeba jukumu la ulinzi

Kusikiliza / Washiriki wa mkutano wa masuala ya ulinzi na usalama mjini Mogadishu nchini Somalia. Picha: UNSOM

Umoja wa Mataifa umetaja mambo ambayo Somalia inapaswa kuzingatia ili hatimaye iweze kubeba jukumu la ulinzi wa nchi hiyo baada ya kumaliza kwa mzozo wa wenyewe kwa wenyewe. Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Michael Keating amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya umoja huo baada ya kumalizika kwa mkutano wa masuala [...]

06/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031