Nyumbani » 04/12/2017 Entries posted on “Disemba 4th, 2017”

Uhakika wa chakula na lishe ni changamoto kubwa Asia na Ulaya:FAO

Kusikiliza / Wakulima Uzbekistan. Picha: FAO

Baadhi ya nchi za Ulaya na Asia ya Kati ni miongoni mwa nchi ambazo zimeathirika zaidi na  mabadiliko ya tabianchi, hali ambayo imesababisha uharibifu wa mazao, misitu na pia kuathiri sekta ya ufugaji na uvuvi. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyozinduliwa leo na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO yenye kichwa "Kuhakikisha [...]

04/12/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa maandalizi kuhusu uhamiaji salama wang'oa nanga Mexico

Kusikiliza / Uhamiaji  salama na wa haki. Picha: UM

Mkutano wa maandalizi kuhusu makubaliano ya kimataifa yanaozingatia uhamiaji  salama na wa haki , umeanza hi leo hadi tarehe 06 Desema ,  katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa mjini Puerto Vallarta Mexico. Mkutano huo ulioleta pamoja washiriki mbalimbali zikiwemo serikali,  asasi za kiraia , Umoja wa Mataifa na mashirika binafsi lengo lake ni kutoa jukwaa [...]

04/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutapata habari za kina kuhusu Yemen Kesho: UM

Kusikiliza / Rais wa zamani wa  Yemen, Ali Abdullah Salehe. Picha: UM/Mark Garten

Umoja wa Mataifa umesema unasubiri taarifa za mjumbe wake maalum kwa Yemen kuhusu taarifa zinazodai kuuawa kwa rais wa zamani wa nchi  hiyo Ali Abdullah Salehe. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amesema hawana taarifa za kina kuhusu habari hizo na kwamba.. (Sauti ya [...]

04/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa msaada wa vifaa vya tiba Libya

Kusikiliza / WHO yatoa msaada wa vifaa vya tiba Libya. Picha: UNSMIL

Shirika la afya duniani  WHO limetoa msaada wa mitambo ya kusaidia kupumua kwa wangonjwa mahututi katika hospitali ya Tragen kusini mwa Libya Msaada huo wa mitambo miwili pamoja na vipuri vyake vyote umetolewa kufuatia kuwepo na upungufu mkubwa wa vifaa hivyo vya tiba kwa wagonjwa mahututi na wenye kuhitaji usaidizi wa kupumua. WHO imeeleza kujizatiti [...]

04/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Saidieni kupambana na uharibifu wa mazingira: Guterres

Kusikiliza / Mkutano Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa unaofanyika Nairobi, Kenya. Picha: UNEP

Tuna haki ya kuishi sehemu salama, tunategemea kula chakula bora, maji safi na kuvuta hewa safi lakini bado tunaendelea kuharibu mazingira. Huo ni ujumbe wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa unaofanyika Nairobi, Kenya. Guterres amesema tayari kuna mbinu na maazimio madhubuti [...]

04/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi

Kusikiliza / UNAIDS HIV

Hii leo tunakuletea jarida maalum linaloangazia harakati za kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi, kwa kuzingatia lengo namba tatu la malengo ya maendeleo endelevu, ya Umoja wa Mataifa, SDGs. Lengo hilo linajikita katika kuimarisha afya na ustawi wa watu wote. Malengo mahsusi ni pamoja na kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030. Umoja wa Mataifa unasema suala muhimu [...]

04/12/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

MachafukoYemen yasababisha misaada kusitishwa: OCHA

Kusikiliza / Mtoto anahudumiwa katika hospitali ya Sab'een huko Sana'a nchini Yemen. Ni mmoja wa watoto waathirika wa kipindupindu. Picha: © UNICEF/UN065873/Alzekri

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA nchini Yemen, Jamie McGoldrick  ameomba kusitishwa kwa utoaji wa huduma za kibinadamu nchini humo baada ya mashambulizi ya hivi karibuni yaliyosababisha vifo vya watu 12 na kujeruhi wengi katika mji mkuu Sanaa. Bwana McGoldrick amesema hali ya usalama kwa watoa huduma wa [...]

04/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia katika ajira kuongeza pato la dunia kwa 26%: Phumzile

Kusikiliza / Uwezeshaji Wanawake utaboresha uchumi. Picha: UN Women

Shirika la Umoja wa Mataifa la wanawake UN Women, kwa kushirikiana  na shirika la maendeleo la wananwake NAMA huko Sharjah Falme za kiarabu, wamezindua kongamano la kimataifa  la siku mbili kuanzia leo tarehe 4 hadi 5 desemba. Lengo la kongamano hilo ni kuhamasisha serikali na asasi za kiraia kuwashirikisha wanawake katika  maendeleo ya kijamii ikiwa [...]

04/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji zaidi wahitajika ili kukabiliana na njaa- FAO

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva. Picha: FAO

Ongezeko la idadi ya watu wenye njaa duniani ni kiashiria kuwa mbinu mpya zahijitaka ili kubadili mwelekeo huo. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva amesema hayo akihutubia kikao cha baraza la shirika hilo mjini  Roma, Italia. Amenukuu takwimu za hivi karibuni zinazoonyesha kuwa idadi ya watu wenye [...]

04/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatma ya uhamiaji wa kimataifa; Macho na masikio vyaelekezwa Mexico

Kusikiliza / Thomas Nguli mmakonde nchini Kenya2

Mkutano wa kuandaa rasimu ya kwanza ya makubaliano ya kimataifa kuhusu uhamiaji unaanza leo huko Puerto Vallarta nchini Mexico, ikielezwa kuwa jambo la msingi ni kuhakikisha makubaliano hayo yanazingatia utofauti wa mahitaji ya wahamiaji kote ulimwenguni. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji wa kimataifa Louise Arbour akizugumza na Idhaa hii [...]

04/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031