Nyumbani » 01/12/2017 Entries posted on “Disemba 1st, 2017”

Wasaka hifadhi na wakimbizi vijana waona nuru huko Ujerumani

Kusikiliza / Muziki umekuwa njia nzuri kwa wakimbizi nchini Ujerumani kuboresha lugha ya Kijerumani. Picha: UNHCR

Stahamala na utangamano ni mambo ambayo Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake ikiwemo lile la wakimbizi duniani, UNHCR unapigia chepuo kila uchao. Hatua hiyo inatatokana na ukweli kwamba mambo hayo mawili ni muhimu wakati huu ambapo idadi ya watu wanaosaka hifadhi ugenini inaongezeka kila uchao. Stahamala huwezesha watu wa rangi,  jinsia au utaifa tofauti kuishi [...]

01/12/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Chanjo milioni 1.4 za homa ya manjano kuokoa maisha Nigeria:WHO

Kusikiliza / Wahudumu wa afya katika kambi ya wakimbizi wa ndani Nigeria. Picha: WHO

Kundi la kimataifa la kuratibu utoaji wa chanjo ya homa ya manjano (ICG) limetoa dozi  milioni 1.4 za chanjo ya homa ya manjano kwa ajili ya kampeni itakayoanza kesho Jumamosi Desemba pili ili kusaidia kudhibiti mlipuko wa homa ya manajano unaoendelea nchini Nigeria. Serikali ya Nigeria kwa msaada wa shirika la afya ulimwenguni WHO na [...]

01/12/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vita, majanga vyaongeza mahitaji ya usaidizi wa kibinadamu

Kusikiliza / Mahitaji ya kibinadamu  yazidi kuongezeka

Kiasi cha dola Bilioni 22 nukta 5 kinahitajika kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2018 unaolenga kuwafikia watu milioni 91. Ombi hilo la fedha limeongezeka kutoka bilioni 22 nukta 2 mwaka jana kutokana na vita, majanga ya asili, milipuko ya magonjwa na kutafuta makazi kusababisha ongezeko la mahitaji ya usaidizi wa kibinaadamu. Mkuu [...]

01/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usaidizi kwa Zimbabwe hadi illipe malimbikizo- IMF

Kusikiliza / Msemaji wa IMF Gerry Rice akizungumza na waandishi wa habari huko Washington DC nchini Marekani. Picha: UM/Video capture

Shirika la fedha duniani, IMF limesema liko tayari kusaidia Zimbabwe kurejea ukuaji wake wa kiuchumi pamoja na utulivu kufuatia kuondoka madarakani kwa Rais Robert Mugabe. Msemaji wa IMF Gerry Rice amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari huko Washington DC nchini Marekani akisema.. (Sauti ya Gerry Rice) "Zimbabwe inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi katika [...]

01/12/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dondakoo wasalia "mwiba" Yemen- WHO

Kusikiliza / Yemen_delivery_Diphtheria

Ugonjwa wa dondakoo unazidi kuwa tishio nchini Yemen baada ya kubainika kuwa hadi sasa hakuna chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitano na kuendelea pamoja na vijana. Shirika la afya duniani WHO linasema ingawa dozi 100,000 za kutibu dondakoo ziliwasili Jumatatu, dawa hizo ni kwa watoto walio na chini [...]

01/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki: Msurupwenye

Kusikiliza / Neno la wiki-MSURUPWENYE

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Msurupwenye".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Nuhu anasema Msurupwenye au ” Overall” ni gauni inayovaliwa kuzuia uchafu unapofanya kazi ngumu kama vile ya matopematope, useremala au ya kiufundi magari.

01/12/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Nuru yaangukia wahamiaji walioteswa Libya

Kusikiliza / Ndege iliyokombolewa IOM inasafirisha wahamiaji 155 wa Guinea, ikiwa ni pamoja na watoto 10 kurudi makwao. Hii ni ndege ya nne tangu Mapema Novemba. Picha: IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, limeanza operesheni ya  kuwarejesha makwao maelfu ya wahamiaji, kufuatia makubaliano baina ya shirika hilo, Muungano wa Afrika, AU, Muungano wa Ulaya, EU na serikali ya Libya. Hatua hii ni baada ya ripoti za vitendo vya kikatili dhidi ya wahamiaji hao ikiwemo unyanyasaji, utumikishaji na kuuzwa utumwani. Wahamiaji [...]

01/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakati maelfu ya Wacongo wakikimbilia Zambia, fedha za misaada zakauka:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa DRC waelekea nchi zinginekufuatia vurugu. Picha: UNHCR

Idadi ya watu wanaokimbia machafuko ya wanamgambo Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na kuingia Zambia sasa imepita 12,000, huku watu zaidi ya 8400 wakiwasili katika miezi mitatu iliyopita. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo, ikiongeza kuwa asilimia 80 ya [...]

01/12/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maisha baada ya vita kwa wapiganaji wa zamani CAR :FAO

Kusikiliza / Wapiganaji wa zamani katika kikao cha mafunzo kwenye mji mkuu wa Bangui, CAR. Mafunzo yanafanyika Bangui katika mikoa ilyoathirika zaidi na vita. Picha: FAO

Zaidi ya wapiganaji wa zamani 1000 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR wamejiunga na mradi unaofadhiliwa na shirika la chakula na kilimo FAO ujulikanao kama "Mradi wa Umoja wa Mataifa" kwa ajili ya upokonyaji silaha, uhamasishaji na ujumuishwaji katika jamii. Selina Jerobon na tarifa zaidi (TAARIFA YA SELINA) Kauli mbiu ya mradi huo ni [...]

01/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM na taasisi ya Panzi na usaidizi kwa manusura wa ukatili wa kingono DRC

Kusikiliza / Wahanga wa ukatili wa kijinsia, nchini DRC. Picha: UM/Marie Frechon

Ukiukwaji mkubwa wa haki za wanawake na watoto ikiwemo ukatili wa kingono na utumikishaji watoto kwenye maeneo ya migodi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC umesababisha Umoja wa Mataifa na wadau wake kuchukua hatua kuepusha zahma zaidi miongoni mwa makundi hayo. Mmoja wa waathirika wa vitendo hivyo amenukuliwa na shirika la uhamiaji la Umoja [...]

01/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila huduma dhidi ya VVU ningalikuwa mfu hivi sasa- Mpho

Kusikiliza / Mpho Tlabaki, mkazi wa Lesotho akitoa ushuhuda wa ugumu wa wanaume kukubali kupima virusi vya ukimwi, VVU. Picha: UNAIDS

Ikiwa leo ni siku ya Ukimwi duniani, ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza harakati dhidi ya Ukimwi, UNAIDS imeonyesha kuwa wanaume ni wagumu zaidi kukubali kupima Virusi Vya Ukimwi, kuliko wanawake. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora Nducha) Huyu ni Mpho Tlabaki mkazi wa Lesotho akitoa ushuhuda wa ugumu wa [...]

01/12/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031