Tuangazie yanayotuweka pamoja badala ya migawanyiko- Ruteere

Kusikiliza /

Mutuma Ruteere, mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa mstaafu akihojiwa na Joseph Msami wa UM. (Picha:UM/Idhaa ya Kiswahili/Assumpta Massoi)

Katika zama za sasa, siasa zinaghubikwa na mwelekeo wa baadhi ya vyama kujipatia umaarufu kupitia ajenda za kibaguzi kutoka kwa wafuasi wao. Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya haki za binadamu imekuwa ikipaza sauti kupinga mwelekeo huo ukisema kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Hoja hiyo na nyingine nyingi ni miongoni mwa mambo ambayo Joseph Msami amezungumza na mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa zama za sasa Mutuma Ruteere ambaye amekamilisha jukumu lake tarehe 31 mwezi wa Oktoba mwaka huu wa 2017. Ruteere katika mahoajiano haya ambayo yanajikita katika lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu amani, haki na taasisi thabiti, anaanza kwa kuelezea changamoto za umaarufu kupitia siasa za kibaguzi.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031