Mpango waanziwa Gambia kusaidia uhamiaji uwe bora zaidi

Kusikiliza /

Kutoka kushoto kwenda kulia, wakiwa na bendera: Fumiko Nagano, Mkuu wa Ujumbe wa Gambia IOM; Mai Ahmed Fatty, Waziri wa Mambo ya Ndani; Attila Lajos, Balozi wa EU na Bulli Dibba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Picha: (IOM) 2017

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya na serikali ya Gambia wanatekeleza mpango wa ulinzi na ujumuishaji wa wahamiaji katika jamii.

Mpango  huo wa miaka mitatu unagharimu zaidi ya dola milioni 4.5 na unatekelezwa wakati huu ambapo idadi kubwa ya raia wa Gambia wanaokimbia nchi hiyo kusaka hivyo Afrika Kaskazini au Ulaya hukwama njiani na hatimaye hushindwa kurejea nyumbani.

Kwa mantiki hiyo Mkuu wa IOM nchii Gambia Fumiko Nagano amesema mpango huo unalenga maeneo matatu ambayo ni kusaidia wahamiaji wa aina hiyo 1,500 warejee nyumbani Gambia na kujiunga tena familia zao na kuendeleza maisha.

Lengo lingine ni kuhamasisha jamii 250 zenye watu wanaoweza kuwa wahamiaji, ili wafuate njia sahihi za uhamiaji na tatu kusaidia mamlaka za kitaifa na kimkoa nchini Gambia kuwa na takiwmu sahihi za uhamiaji ili kusaidia sera za mipango ya maendeleo.

Kupitia mpango huo ambao IOM Inatekeleza kwa kushirikiana na serikali, wahamiaji wataamua wenyewe kuhamia ugenini kwa hiari badala ya kuwa ni kitu cha lazima.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930