Kesi ya ukatili kwa watoto DRC yaanza kusikilizwa leo huko Bukavu

Kusikiliza /

Mahakama ya kijeshi huko Bukavu jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Picha: MONUSCO

Mahakama ya kijeshi huko Bukavu jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC leo alhamisi inaanza kusikiliza kesi ya watuhumiwa 18 wanaoshtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kibinadamu dhidi ya watoto wapatao 51.

Yadaiwa kuwa watu hao waliokuwa wamejihami walitenda uhalifu huo kati ya mwezi mei mwaka 2013 hadi mwaka 2016 kwenye eneo la Kabare ambapo watoto hao walikabiliwa na ukatili na wawili kati yao walifariki dunia.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO ndio unafadhili usikilizaji wa kesi hiyo kwa kutumia mfumo wa gari ambalo linatembea kutoka eneo moja hadi jingine kusikiliza kesi na ushahidi ambapo kesi inatarajiwa kuendelea hadi tarehe 26 mwezi huu.

Usaidizi huo wa MONUSCO umeweka pia mazingira ya ulinzi kwa wahanga 46 wa tukio hilo na mashahidi wao ili kuhakikisha kuwa hawana hofu ya kushiriki kwenye kesi hiyo.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031